Maisha ni kama mpira wa miguu. Katika nafasi kumi na moja kila mmoja anacheza kwenye nafasi yake.

Ili ufanikiwe sio lazima uwe sehemu ya kufunga goli. Unaweza kuwa golikipa mwenye mafanikio makubwa, unaweza kuwa beki mwenye mafanikio makubwa pia.
Swali linakuja kwako unaitumiaje nafasi yako? Nafasi uliyopewa kuicheza ndio inakufaa kabisa kufanya mambo makubwa hata ukachukua tuzo.
Ukibaki unasema ningepewa namba tisa ningefanya vizuri hautakaa ufike hapo ulipo. Acha kupoteza muda kusubiria namba tisa tumia namba unayochezea sasa kuonyesha yaliyopo ndani yako.
Hata kama wewe  namba tisa  ndio unaiweza Zaidi kweli huwezi kupewa kama hujaweza kuitumia vizuri namba uliyonayo sasa hivi.
Jiulize leo unatumia ipasavyo nafasi uliyonayo? Siku ukinyang’anywa utaondoka ukilalamika?
Kila mmoja ana nafasi sehemu mbalimbali kama kazini, kwenye familia, kwenye biashara na kwenye jamii inayotuzunguka. Kama kila mmoja akiweza kutumia nafasi aliyonayo vyema tunaweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye dunia ya sasa.

Usisubiri usukumwe, usisubiri uibiwe ndio uwe makini, usisubiri mtu aje akuambie cha kufanya. Ifahamu sehemu uliyosimama itumie vyema kuacha alama. Usingoje upandishwe cheo ndio uanze kuonyesha ujuzi wako wa kazi. Usingoje ulalamikiwe kwamba ni mzembe ndio uanze kufanya kazi kwa bidii.
Fahamu majukumu yako kwenye kila nafasi uliyonayo na uwajibike. Kila mmoja ana nafasi kwenye Maisha yake binafsi, familia, jamii na sehemu ile anayofanya kazi. Sehemu hizi ni za muhimu sana kwenye Maisha yetu kama kila mmoja atawajibika ipasavyo tutapata kile tunachokitaka.
ZIMEBAKI SIKU CHACHE TUTAFUNGA ZOEZI LA USAJILI WA SEMINA JIUNGE HAPA…

Jipatie nakala yako ya Kitabu Siri 7 za Kuwa Hai Leo piga 0654726668

Karibu sana.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255654726668

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading