HATUA YA 114: Kama Unaendesha Biashara na Huna vitu Hivi Unapotea…

jacobmushi
2 Min Read
Kama unamiliki biashara ambayo una malengo ya kufika mbali, yaani kuwafikia watu wengi Zaidi ya ulio nao sasa hivi na bado hujamiliki mtandao unapoteza muda wateja wengi sana.

Dunia imebadilika sana na kwa sasa tunahama kutoka kwenye mifumo ya analogia kwenda digitali. Kama utashindwa kubadilika na mifumo hii inavyobadilika utakuwa unakosa vitu vingi sana.
Njia za kutangaza biashara zako zimekuwa rahisi sana kuliko unavyofikiri. Sasa hivi unaweza kuwafikia watu wengi sana kwa njia rahisi sana ukiwa na simu yako ya mkononi.
Kwanza unahitaji ukurasa wa biashara wa facebook ukurasa huu utakuwa ni kwa ajili ya kuitambulisha biashara yako. Utabeba maelezo ya namna unavyoendesha biashara yako na mahali ilipo.
Sehemu ya pili unahitaji ukurasa wa Istagram ambapo huku Zaidi utakuwa unaweka picha za bidhaa zako au huduma unazotoa.
Ukishakuwa na kurasa hizi mbili ndio unakuwa mwanzo wa wewe kuanza kuitambulisha biashara yako sehemu mbalimbali duniani. Watu wengi wataanza kukufuatilia na wengine watakuwa wateja wako.
Kitu cha tatu unatakiwa umiliki blogu ambayo itabeba maelezo yote ya biashara zako na huduma unazotoa.
Sasa hivi karibu kila unaekutana nae kila siku ana simu inayomwezesha kutumia mtandao wa intaneti. Hii ni fursa ya kipekee kwa mtu yeyote yule hata kama sio mfanyabiashara kuweza kuwafikia watu wengi kupitia kile anachokifanya.
Kama mpaka sasa huna hata kimoja kati ya nilivyotaja hapo juu unahitajika kuchukua hatua haraka sana. Popote ulipo chukua hatua na uanze kuiendea dunia kupitia mtandao.
Kitu cha mwisho ukimiliki vitu hivyo haimaanishi ndio utaanza kutengeneza pesa hapo kwa hapo tutaanza kujifunza pamoja ni jinsi gani unaweza kutumia vyema vitu hivyo ili uweze kuwafikia watu wengi Zaidi.
Kumiliki Vitu Hivi Bonyeza Hapa.
Karibu sana
Your Partner in Success
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
jacobmushi.com.
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading