Hakuna kitu ambacho hakina chanzo. Ukiwa na hasira sana lazima kuna kitu kimesababisha uwe na hasira. Vile vile ukiwa na furaha lazima ujue chanzo cha furaha.

Hapa kwenye kutafuta chanzo cha furaha ndio kunakuwaga na matatizo mengi sana kwani wengi hawajui ni wapi wanaishia kutafuta furaha Maisha yao yote. Siku zote furaha ikiwa inaletwa na vitu ambavyo vinaisha au vinavyobadilikabadilika utajikuta Maisha yako yote unaitafuta furaha.
Watu wengi wanakunywa pombe kupindukia wanakosa furaha.
Watu ambao wanakuwa makatili na kudhuru binadamu wengine au Wanyama wamekosa furaha.
Mtu yeyote anaefanya vitendo viovu haiwezekani akawa anapata furaha kwasababu furaha ya kweli haipo katika kufanya maovu bali ni kwa kufanya yaliyo mema.
Furaha ya kweli inatakiwa iletwe na kazi unayoifanya. Kazi unayoifanya inatakiwa iwe ile uliozaliwa kuja kuifanya hapa duniani.
Furaha inayotokana na kufanya kazi ambayo umeitwa kuja kuifanya hua haipotezwi kirahisi na vitu vya kupita.
Vipo vitu vingi vinaweza kutumika kama vichocheo vya furaha lakini havitakiwi viwe vyanzo vya furaha. Tunapokosea ni pale tunapotaka vichocheo vya furaha viwe vyanzo vya furaha zetu.
Kama wewe vichocheo vya furaha  ndio vimekuwa vyanzo vya furaha, Maisha yako yatakuwa magumu sana. Furaha hailetwi na watu wanaokuja kwenye Maisha yetu bali inaweza kuongezwa. Furaha haitwi na vitu tunavyovinunua madukani bali inaweza kuchochewa.
Kama ulikuwa kwenye mahusiano na mtu akakuacha halafu ukasema ameondoka na furaha yako utakuwa unakosea sana. Mtu yeyote hayupo kwenye Maisha yako kukuletea furaha bali kuongeza furaha uliyonayo. Akiondoka atakuacha na furaha yako.
Chanzo cha Furaha kipo ndani ya Kazi iliyokuleta hapa duniani. Hii haiwezi kuondoka hadi siku unaondoka wewe, chanzo cha furaha kipo kwenye vitu ambavyo Mungu ameweka ndani yako. Furaha itakuja wakati ukianza kuviishi vitu hivyo.
Jipatie nakala ya Kitabu cha Siri 7 za Kuwa Hai Leo wasiliana nami kwa 0654726668

Kwa huduma mbalimbali ndani ya mtandao huu bonyeza hapa
Karibu sana.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255654726668

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading