Habari ya Leo Msoma wa Makala za #Hatua za Mafanikio. Ninapenda kukushukuru sana kwa kuwa mmoja wa watu ambao mmeamua kuwa nyuma yangu. Napenda kuwashukuru sana wote wale mlioamua kusoma Makala hizi kila siku ya asubuhi.

Ninayo furaha kubwa sana kwani leo ni siku ambayo nimetimiza miaka 25 tangu niwepo hapa duniani. Nimeamua kuitoa siku ya leo kuandika Makala hii ya shukrani zangu kwa wasomaji wangu leo kwasababu nimetimiza robo karne ya kuwepo hapa duniani.
Bado safari ni ndefu tunakoelekea ni pazuri sana.
Shukrani zangu za dhati zikufikie wewe unaesoma Makala hizi na kuzitendea kazi kwani kuna siku moja utakuja kuwa mmoja wa watu wakuu katika dunia hii.
Shukrani zangu za dhati zikufikie wewe ambaye huchoki kusoma Makala hizi kila siku kwani unanipa moyo na hamasa ya kuendelea Zaidi.
Shukrani zangu za dhati zikufikie wewe unaenitumia ujumbe wa mara kwa mara kwa kusema umebarikiwa na Makala Fulani iliyokugusa sana, unaniongezea nguvu.
Shukrani zangu za dhati zikufikie wewe unaesambaza Makala hizi kwa marafiki zako ili wapate vitu vizuri ambavyo wewe umevifaidi.
Shukrani zangu za dhati zikufikie wewe uliyesema hutaishia njia hadi uitimize ndoto yako.


Hivyo basi kwa siku hii ya leo na ya kipekee sana kwangu ningependa kusema kwamba Ashurkuriwe Mungu aliesema nizaliwe duniani katika kipindi hiki ambacho wanadamu wanahitaji maarifa kuliko kipindi kingine chochote.
Ninao wajibu wa kuhakikisha wewe unapiga hatua kwenye kile unachokifanya ili kufikia mafanikio. Na hili ndilo hasa lililonileta duniani. Huwa nasema ni heri nikose vyote lakini nisiache kuandika maandishi haya ambayo yanawagusa wengi humu duniani.
Karibuni sana.
Jipatie Nakala ya Kitabu nilichoandika kiitwacho Siri 7 Za Kuwa Hai Leo wasiliana nami kwa 0654726668.

Jipatie Bidhaa na Huduma mbalimbali ndani ya mtandao huu kwa kubonyeza hapa……

Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: 0654726668
jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading