Habari ya leo mwanamafanikio mwenzangu.  Napenda Niwashukuru wote mlioshiriki katika kunitakia heri ya siku yangu ya kuzaliwa jana. Nimepokea jukumu la kuongeza thamani Zaidi kwenu. Upendo mliouonyesha umekuwa ni deni kwangu. Natakiwa kurudisha upendo maradufu.
Yapo mambo mengi hua yanaendelea kwenye biashara nyingi za watu ambayo kwa kawaida mtu yeyote anaetoa pesa zake ili kulipia huduma au bidhaa hawezi kufurahia kufanyia. Lakini kwasababu ya wengi kutokujua ama uzembe binafsi wanaendeleza kufanya hayo. Mwisho wa siku ni pale biashara inapoyumba na wateja kupotea mtu anakuja kushtuka kumbe ni yeye mwenyewe alikua anawafukuza bila kujua.
Kutokujali Malalamiko.
Ukiona mteja wako analalamika kwa jambo lolote kwenye biashara yako wewe kama mmiliki unatakiwa ujue jukumu lako ni kutatua malalamishi ya wateja. Wateja hawa wakiona wanachokilalamikia hakitatuliwi mwisho wa siku watatafuta mtu mwingine. Bahati mbaya sana ni mara chache sana ukakuta biashara yako ni wewe mwenyewe unaifanya.
Kingine kibaya ni kwamba wateja hawa wakiondoka na malalamishi haya wataenda kuyasema kwa marafiki zao. Na kama watafanya hivyo ujue biashara yako inapoteza wateja kabisa.
Nimekuwa nawasikia watu wengi wanaambiana, “Pale kwa kina Fulani ni wazembe sana hawajali wateja” “pale ni wachafu sana” “Pale ukienda na pesa kubwa watakusumbua” na mengine mengi.
Kama mfanya biashara mwenye maono hakikisha unahusika katika kutatua malalamishi ya wateja wako.
Kutokuwa karibu na wateja wako.
Hakuna mteja ambaye hapendi kuonekana wa maana. Yaani mteja kupata ile huduma ambayo itamfanya aone pesa yake imethaminiwa. Kama wewe mar azote ukishachukua pesa ya mteja basi habari ndio imeisha basi ujue unakwenda kumpoteza. Mteja anapenda atabasamu kwenye biashara yako. kitu ambacho hutakiwi kusahau ni kwamba mteja wako hela anayoitoa aliitafuta kwa ugumu kuliko hata wewe unavyoichukua mkononi mwake. Hivyo ni muhimu sana umfanye ajisikie hajapoteza pesa yake.
Kubagua wateja.
Kuna tabia ya kuwabagua wateja kwenye biashara mfano mtu amekuja akanunua vitu vya elfu moja, wakati unamhudumia akaja mwingine ambaye hua ananunua vitu vingi vya pesa nyingi. Wewe ukaacha kummalizia yule wa elfu moja ukasema ngoja nimhudumie huyu anaetoa pesa nyingi. Hayo ni makossa makubwa sana. Hakuna mtu ambaye pesa yake haina thamani. Alienza amaliziwe kuhudumiwa kwanza.
Ubaguzi mwingine ni ule unamfanyia vizuri yule unaemjua kuliko yule mgeni. Yaani wamekuja watu wawili kwenye biashara yako  mmoja unamfahamu ni rafiki yako mwingine ni mgeni. Rafiki yako ukampendelea Zaidi ukamfanyia vizuri kuliko yule mgeni wakati wote wamechukua vitu vinavyofanana. Kikawaida mteja huyu hatarudi tena hapo dukani kwako. Unatakiwa ujue namna ya kuwahudumia wateja wako bila kuwabagua. Kama ni ubora wa huduma uwe kwa wote haijalishi ni kiwango gani cha pesa mtu ametoa.
Karibu sana.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading