HATUA YA 118: Mambo Ya Kuzingatia kwa Wajasiriamali Wadogo

jacobmushi
3 Min Read
Habari ya leo msomaji wa www.jacobmushi.comleo katika HATUA tutaangalia kwa ufupi mambo ya kuzingatia kama mjasiriamali. Ili uweze kusonga mbele na ufikie kwenye kuitwa mtu Fulani mkuu lazima ujue vitu ambavyo ni vya muhimu kama msingi wa mafanikio yako.

Uaminifu.
Uaminifu ndio msingi wa kwanza kwa kila mtu ambaye anaingia kwenye ujasiriamali.  Bila uaminifu huwezi kukaa kwa muda mrefu kwenye soko. Uaminifu tunaouzungumzia hapa ni jinsi unavyosema na unavyotekeleza. Kama umeawaahidi wateja wako kwamba bidhaa zako ni nzuri sana basi hakikisha zinakuwa hivyo. Umeahidi huduma bora basi hakikisha unatekeleza kwenye kila unachokifanya.

Wakati mwingine kinachowashinda wengi ni kuwa wawazi. Haijalishi umepitia changamoto za aina gani kama utashindwa kuwa muwazi kwa wateja wako watakuona tapeli. Pia ili kujenga uaminifu Zaidi na wateja wako lazima ujenge tabia ya kuwasiliana nao mara kwa mara. Kama huna mawasiliano nao wateja wako kuna mwingine atakuja na atawachukua.


Ubunifu.
Ubunifu unaingia kwenye kila kitengo, lazima ujue namna ya kuwa karibu na wateja wako. Usifanye kama wengine wanavyofanya. Lazima ujue namna ya kufanya bidhaa yako iwe bora Zaidi. Lazima ujue namna ya kuongeza vitu vipya kwenye bidhaa zako ili kuwapata wateja Zaidi.

Kama utashindwa kuwa mbunifu na kuja na vitu vipya ambavyo vitamshangaza mteja atakuzoea na mwishoe kukuona kama wengine. Hakikisha unakuwa unacho kitu kinachokutofautisha na wengine.

Jifunze kila siku.
Kama mjasiriamali kujifunza kwako ni lazima. Ili uweze kuwa mbunifu,uzishinde changamoto. Na mengine mengi huwezi yote hayo kama hujifunzi. Tunaposema kujifunza zipo njia nyingi za kujifunza kama kusoma vitabu. Kujifunza kwenye Makala kama hizi ninazoandika kila siku. Jifunze kwa wengine hakikisha unapata muda wa kutembelea wenzako uone wanafanya nini cha tofauti.

Teknolojia inatupa nafasi kubwa ya kuweza kujifunza na kuona mambo mapya kirahisi Zaidi. Popote ulipo unaweza kuona mambo mapya yanayoendelea sehemu mbalimbali duniani. Usikubali kuwa wa kawaida usikubali kubakia hivyo ulivyo.

Karibu sana
Jipatie Nakala yako ya Kitabu cha Siri 7 za Kuwa Hai Leo Wasiliana nami kwa 0654726668.

Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668
Email: jacob@jacobmushi.com
Blogs: www.jacobmushi.com
jacobmushi.com
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading