Uwezo wa kufanya maamuzi haraka unategemeana na mtu anavyojitambua na kule anapoelekea.

Mara nyingi mtu anaweza kuwa na wasiwasi wa kufanya maamuzi kwasababu hajaelewa ni wapi anapoelekea.
Kama umeweka malengo ambayo yanaeleweka katika utendaji wake huwezikusitasita wakati unataka kuamua kufanya jambo Fulani.
Hii  ni kwasababu unajua ni kitu gani kinakufaa na kitu gani hakikufai. Ndio kuna wakati hatuwezi kubashiri mambo kwa uhakika lakini kuna baadhi ya mambo ambayo unaweza kuyafanyia maamuzi haraka kulingana na jinsi yalivyo.
Ukitaka kutengeneza uwezo wako wa kufanya maamuzi unatakiwa ujipe changamoto mbalimbali ambazo zinakufanya ufanye maamuzi.
Unapokuza uwezo wako wa kufanya maamuzi unajipa nafasi ya kuweza kusimamia mambo makubwa.


Kama utakumbuka kipindi cha nyuma kuna baadhi ya mambo ulikuwa huwezi kufanya hadi ukaulize kwa mtu aliekuzidi umri au mwenye uwezo mkubwa kuliko wewe.
Lakini kadiri tunavyokuwa ndio tunatakiwa tuwe na uwezo wa kufanya maamuzi kwenye baadhi ya mambo bila kwenda kuomba ushauri mahali Fulani.
Kuna baadhi ya mambo ukiomba ushauri yanaonyesha jinsi ulivyo na uwezo mdogo wa kufanya maamuzi kwenye Maisha yako, hivyo ni muhimu sana ujijengee tabia ya kutatua matatizo kwa kufanya maamuzi wewe mwenyewe.
Kadiri unavyoweza kutatua matatizo pekee yako ndio unavyozidi kuongeza uwezo wako wa kuwaongoza wengine.
Watu wengi waliokosa maono na malengo hawana uwezo wa kufanya maamuzi kwenye baadhi ya mambo kama wao lazima wawategemee wengine.
Ukijua unachokitaka utaweza kuamua kama jambo Fulani linafaa au halifai, na hapa utakua unatazama lina mchango gani kwenye maono yako au malengo yako.
Karibu sana.



Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668
Email: jacob@jacobmushi.com
Blogs: www.jacobmushi.com
jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading