HATUA YA 120: Wewe Ni Nani?

jacobmushi
2 Min Read
Hili ni moja ya swali ambalo wengi wakiulizwa huwa wanapata kigugumizi kujibu. Lakini leo nataka uondoe kigugumizi hicho.

 

Wewe ni nani? Ulishawahi kusikia watu wanaulizana, Hivi huyu Jacob Ni nani? Tayari wameshataja jina lakini wanajiuliza ni nani. Unajua wewe sio jina lako. Wewe unatambulishwa Zaidi na ile kazi iliyoko ndani yako.
Ni muhimu sana kujijua wewe ni nani ili unapojitambulisha usifanye makossa ya kutokujisema wewe ni nani. Kuna sehemu unaweza kufanya jambo watu wakabaki wana maswali kichwani wanajiuliza huyu mtu ni nani hasa?
Leo naataka ujiulize mwenyewe kwanza wewe ni nani? Ukishapata jibu anza kufanyia kazi huyo wewe hadi watu waanze kujiuliza wewe ni nani. Watu wataanza kujiuliza wewe ni nani kwasababu ya matendo yako.
Soma: Mambo 7 Yanayoonyesha Unachokifanya sio Kusudi Lako
Unatakiwa ufanye jambo lililokuleta hapa duniani hadi watu wakisikia jina lako wanapata jibu moja kwa moja wewe ni nani. Unatakiwa uwe na neon moja linalokutambulisha.
Ugumu upo kwenye kugundua wewe ni nani. Hapo ndipo hatua ya kwanza ilipo hayo mengine yanafuata. Ukishajua wewe ni nani unapata mwangaza mpana wa kule unapotaka kufika. Ukishajua wewe ni nani unaweza kutengeneza picha kubwa sana ya vile unavyotaka kuja kuwa au kutambulika na dunia.
Anza hapa kwenye ugumu. Kila siku asubuhi ukiamka jiulize hivi mimi ni nani? Nimekuja duniani kufanya nini? Kabla hujalala jiulize maswali hayo. Kwa kujiuliza maswali utagundua majibu taratibu na mwisho utaanza kuona maana ya Maisha yako hapa duniani.
Kujifunza Zaidi na kujua wewe ni nani Jipatie nakala yako ya Kitabu cha Siri 7 za Kuwa Hai Leo wasiliana nami kwa 0654726668

 

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading