HATUA YA 123: Waambie Wasikupangie

Wewe ndio unajua unakoelekea kuna wakati unaweza kufanya mambo huku unawaza watu wanasemaje. Mfano watu wengi tafsiri ya mtu mwenye mafanikio ni mwenye gari au aliejenga nyumba yake nzuri. Lakini tafsiri ya mafanikio kwako wewe unatakiwa uitengeneze mwenyewe.

Ukishindwa kuwa na maana yako ya mafanikio kutokana na yale unayoyafanya Maisha yako yanaweza kuwa ya kuwaridhisha wengine. Kama wao wanadhani kuwa gari ndio mafanikio basi itakubidi wewe ujiumize sana ili uwe na gari.

Waambie wasikupangie lini utaoa au kuolewa umri umeenda ndio lakini hutakiwi kukurupuka. Haijalishi watu wanataka uwe vipi inajalisha Zaidi vile ambavyo wewe unaona.

Binadamu tumejenga picha ambayo ni tafsiri ya mtu mwenye mafanikio ndio maana jamii nzima inakuwa inaishi Maisha ya kufanana yasiyo na mabadiliko.
Ulipokuwa shule uliambia soma kwa bidii uje kuwa na Maisha mazuri. Vilevile ukaonyeshwa wale walio mtaani baada ya kufeli Maisha yao yalivyo magumu. Hapo na wewe ukaamini kwamba Maisha mazuri yanaletwa na kusoma kwa bidii.

Sasa hivi wanajua una Maisha mazuri baada ya kupata kazi, lakini wewe ndie unajua kama hayo ni Maisha mazuri unayoishi au unaishi Maisha ya kuwaridhisha hao waliokwambia ukisoma utakuwa na Maisha mazuri.

Ili uweze kutoka kwenye hilo gereza lazima uamue kubadilika, tengeneza maana halisi ya Maisha yako. tengeneza misingi ambayo utaifuata hadi ufikie ile picha yako kubwa. Usikubali kuyumbishwa na tafsiri za watu wengine juu ya maana ya mafanikio na Maisha.

Jipatie Nakala ya Kitabu cha Siri 7 za Kuwa Hai Leo, Wasiliana nami kwa 0654726668.


Karibu sana.
Jacob Mushi.
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668
jacobmushi.com.
jacobmushi
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue Reading