Habari rafiki yangu. Karibu katika hatua ya leo ya mafanikio.

Ndugu Zako Wa Karibu.
Hawa ni watu wa kuwa nao makini sana kwasababu wanaweza kuwa sababu yaw ewe kurudi nyuma. Kuna wakati unaweza kuhitaji ushirikiano wao labda mchango wa mawazo au pesa ili kukamilisha jambo Fulani wakashindwa kukuelewa.
Inawezekana sababu ikawa ni hawaamini kile unachokwenda kukifanya kama kitaleta matokeo au hawajakuelewa.
Jitahidi sana waelewe vyema kule unapoelekea hata kama hawataamini lakini siku moja usije kubeba lawama kwao kwamba hukuwafahamisha vyema kule unapoelekea.
Ni muhimu wakafahamu pia kwamba una majukumu gani ili kuepuka lawama za wewe kuwa bize kupita kiasi.
Marafiki Zako.
Hawa ni watu ambao unawaeleza mambo yako ya ndani au ya siri wakati mwingine. Hawa wanapaswa kufahamu pia kule unapokwenda. Na hawa wanatakiwa wawe marafiki ambao tayari umeshawafahamu vyema kama wanakufaa kwenye ndoto zako au lah.
Hawa kuwa nao makini sana na uhakikishe wanatambua yale mambo ya muhimu ili unapokwama waweze kutoa ushirikiano. Kuna wakati unaweza kuwafata kuomba msaada Fulani wa kipesa au hata ushirikiano wakasema wewe mambo yako unafanyaga peke yako huwashirikishi hadi upate shida.
Kuepuka lawama hizi hakikisha wanafahamu pia unapokwenda na kile unachokifanya.
Mpenzi/Mwenzi.
Mpenzi/mwenzi wako anaweza akawa sababu ya kukurudisha nyuma kama asipoelewa vyema kule unapoelekea. 
Atashindwa kukutia moyo unapopitia magumu.
Atashindwa kuonyesha kujali kile unachokifanya kwakua hajui vyema kule unapokwenda.
Atashindwa kutoa ushirikiano wa kutosha hasa ule wakati unapomhitaji sana.
Ili kuepuka haya yote jitahidi sana aelewe vyema kule unapoelekea, jitahidi sana aelewe vita unayokwenda kupigana. Hapa utampa nafasi ya kuweza kukushauri na kukutia moyo badala ya kukulaumu au kulalamika kwamba haumpi muda wa kutosha.
KUMBUKA:
Watu hawa kila mmoja ana nafasi yake. Sio kila jambo utawaeleza lazima ujue namna ya kusema na mtu. Kuna mengine utabakiza moyoni mwako kuepusha kukatishwa tamaa. Hivyo ni muhimu sana ujue lipi la kusema na lipi ulipe muda kwanza.
Jipatie Nakala ya Kitabu cha Siri 7 za Kuwa Hai Leo, Wasiliana nami kwa 0654726668.


Karibu sana.
Jacob Mushi.
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading