HATUA YA 125: Kwanini Usiwe Wewe?

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read
Kama kwenu hakuna mtu mwenye mafanikio kabisa kwanini usianze kuwa wa kwanza?

Kama kwenu hakuna mtu maarufu hata mmoja kwanini usianze mchakato wa wewe kuwa wa kwanza?
Kama kwenu hakuna aliewahi kusoma kafika chuo kikuu kwanini wewe usiwe wa kwanza?
Badala kulalamika unaweza kubadilisha ule udhaifu unaouona kuwa fursa. Badala ya kutoa sababu kedekede za wewe kushindwa badili sababu hizo ziwe fursa ya kukutoa hapo ulipo.
Kama kwenu hakuna hata ndugu mmoja anaeweza kumsaidia mwenzake wewe ndio unatakiwa upambane ili uje kuwa ndugu wa kwanza anaeweza kuwa mfano wa kuigwa kwa kuwasaidia wenzake.
Kama mahusiano mengi yanavunjuka ama kuvurugika kwa sababu ya hizi simu kwanini wewe usiwe wa kwanza kuzitumia simu vizuri ili kutunza mahusiano yako?
Kama viongozi wengi wanawaza matumbo yao kwanini wewe usiwe kiongozi wa kwanza mzalendo alieweka tumbo pembeni kwanza.

Kama umekuwa wa kwanza kuona tatizo basi wewe ndie mwenye suluhisho. Hukuona tatizo bure nafasi ya kuona tatizo ni nafasi ya kutoa utatuzi.
Ninachoweza kukwambia leo hizo sababu zote unazotoa ni fursa ambazo ukiweza kuzitumia vizuri utatoka kabisa.
Tatizo linakuja pale wewe mwenye hizo fursa unabaki unalalamika na kutoa sababu nyingi za kushindwa.
Kama kwenu watoto wa kike huwa hawaolewi wanaishia kuzalia nyumbani hiyo ni fursa kwako kutokuwa mmoja wao.
Kuna watu wanasema watoto waliokosa malezi ya wazazi wawili wanakuwa na tabia mbovu embu kuwa wewe wa kwanza mwenye tabia njema.
Itumie vyema nafasi ya wewe kuona tatizo kwa kuleta suluhisho.
Jipatie Nakala ya Kitabu cha Siri 7 za Kuwa Hai Leo, Wasiliana nami kwa 0654726668.


Karibu sana.
Jacob Mushi.
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668
jacobmushi.com.
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading