Fedha hazikai kwenye mifuko iliyotoboka.

Vitu vya thamani haviwekwi kwenye mifuko iliyotoboka.

Mwenye Mifuko iliyotoboka anaishi kwa wasiwasi maana muda wowote akijisahau anaweza kupoteza vitu vyake vya thamani.

Usikubali kuwa mtu mwenye mifuko iliyotoboka.

Mifuko ninayozungumzia mimi ni mifuko iliyondani ya ufahamu wako. Kama ufahamu wako kwenye upande wa fedha umetoboka huwezi hata siku moja kuivumilia pesa iliyoko mfukoni kwako.

Mifuko yako ya ufahamu juu ya pesa ikiwa ina matobo pesa zako zote zitaishia kwenye matumizi ya anasa na starehe.

Ni kweli kila mmoja ambaye kwa sasa hana pesa anatamani na anawaza siku akipata pesa nyingi atazitumia kwa namna mbalimbali. Lakini pesa nyingi hazijagi kwa pamoja. Pesa nyingi ni mkusanyiko wa pesa kidogo kidogo unazokusanya kila siku.

Soma: Tumia Nguvu ya Ubongo wako Kuwa Tajiri

Tatizo linalofanya wewe usisonge mbele ni kwamba una mifuko iliyotoboka.

Mifuko iliyotoboka haifai kuwekea akiba.

Hakikisha unayatambua matobo uliyonayo na ufanye mpango wa kuyaziba ili mifuko yako ijae fedha.

Matundu haya yanaweza kuwa ni matumizi mabovu ya pesa, tamaa, kununua nunua vitu hovyo.

Embu jiangalie ni vitu vingapi ambavyo unafanya na havina maaana sana. Kama kuna vitu vinatumia pesa kila siku kutoka mfukoni kwako na vitu hivyo ukiviacha hakuna madhara yeyote yanayoweza kutokea bora uviache maana havina umuhimu.

Mfano una tabia ya kunywa soda au bia kila siku, jiulize ukiacha kunywa utapata madhara gani? Kuna kitu gani kitapungua kwenye mwili wako?

Ziba matundu ya mifuko yako ya fedha kwa kupunguza vitu ambavyo havina tija kwenye Maisha yako.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading