Ni kweli Ng’ombe hachoki kutoa maziwa lakini  lazima kwanza awe anapata chakula cha kutosha kila siku.

Kuku hachoki kutaga kila siku lakini ili aweze kutaga kila siku lazima apate chakula cha kutosha kila siku.
Maana yake ni kwamba hakuna matokeo ambayo yanakuja bila kuwepo kwa gharama nyuma yake. Ili uweze kufikia ukuu au ndoto yako lazima kuna gharama unatakiwa uilipe nyuma ya pazia.
Ukiona watu wamefanikiwa kwenye yale mambo walioamua kuyafanyia kazi lazima utambue kuna kitu wanafanya kila siku nyuma ya pazia ili waweze kubakia huko juu walikofika.
Usidanganyike kwamba huko juu unakokwenda kuna mahali utakuwa unapumzika na kustarehe tu. Lazima kuna gharama ambayo utakuwa unailipa kila wakati ili uendelee kung’ara.

Makossa makubwa ambayo tunayafanya ni kujisahau tukifikiri tumeshapata kile tunachokitaka. Tunasahau kumpa ng’ombe wetu majani au pumba kwa wingi tukifiri ataendelea kutoa maziwa.
Tunasahau kwamba haijalishi kuku amefikia uwezo wa kutaga mayai mengi kiasi gani, ili aendelee kutaga lazima apatiwe chakula ashibe kila siku.
Unapofika kwenye kilele cha mafanikio ukasahau kujifunza, ukasahau vile vitu ulikuwa unafanya kila siku hadi ukafika hapo ulipo lazima uanze kuporomoka.
Na kawaida ni kwamba ng’ombe akishakosa chakula kwa muda mrefu hata maziwa atakayoyatoa hayatakuwa na matamu kama zamani. Hapo unaingia hatari ya kukimbiwa na wateja wako wa maziwa.
Usije ukajisahau rafiki yangu. Popote pale ulipofika endelea kuweka bidii na juhudi, usiwadharau wengine.
Jipatie Nakala ya Kitabu cha Siri 7 za Kuwa Hai Leo, Wasiliana nami kwa 0654726668.

Karibu sana.
Jacob Mushi.
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading