Hapo zamani kabla ya kutambua ni kitu gani natakiwa kufanya ili nifikie Mafanikio nilizoea kusema ipo siku ndoto yangu itatimia.
Ni maneno mazuri sana na ya kutia Moyo lakini kama hakuna unachofanya hiyo ndoto itabakia kuwa ndoto.

Ipo siku utatambua haya ninayosema ni Kweli. Huwezi kusubiria mazao wakati hakuna shamba lolote ulilootesha mbegu.
Ili neno ipo siku liwe na maana wewe Rafiki anza leo Kutafuta ni mbegu gani unatakiwa uoteshe ili uweze kuja kuvuna hayo unayotamani kuona kwenye maisha yako.
Ipo Siku usiyoijua utakumbuka haya maneno kwamba lazima usubirie kitu ambacho umekifanyia kazi. Hakuna neno jingine lifaa kukueleza zaidi ya hilo.
Kama unafikiri ipo siku utampata mpenzi mwaminifu halafu hakuna unachofanya sasa hivi ili uyo mpenzi atokee hiyo ni ndoto.
Kama unadhani kuna siku utakuwa tajiri ni Vizuri sana lakini kama hakuna unachokifanya ili kufikia utajiri, utaendelea kusubiri.
Lazima tuambiane Ukweli. Kwani Ukweli utatuweka huru kwenye vifungo vya umaskini na fikra. Mimi kazi yangu ni kukuonyesha njia na vitu ambavyo unatakiwa kufanya. Kama utakuwa tayari kufanyia kazi haya utaona matokeo yake.
Hakikisha kuna kitu umefanya na unaendelea kukifanya ili utimize kile unachotamani kitokee.
Karibu sana.
Jacob Mushi.
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
Email: jacob@jacobmushi.com

jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading