Kwenye dunia ya sasa tunaelekea kwenye kipindi ambacho kila kitu unachokifanya kuna mwingine anafanya. Kama ni biashara unafanya kuna mwingine anaweza kufanya kama wewe.
Kutokana na hali ya kila mmoja kuweza kumiliki biashara yake, kumekuwa na changamoto kubwa sana ya watu kutotambua ni vitu gani wafanye ili kubakia kwenye soko na kukua Zaidi. Ukweli ni kwamba kama biashara unayoifanya kuna mwingine anaweza kuifanya hata leo basi kila mmoja yupo kwenye hatari kubwa sana.
Kila mmoja yupo kwenye hatari kama hatatambua ni vitu gani vya muhimu ambavyo vitamfanya aendelee kuwepo sokoni.
Haijalishi una bidhaa bora kuliko wote hapa nchini kama utashindwa kumjali mteja wako huwezi kukua hata siku moja.
Soma:
Tunapozungumzia kumjali tumebeba maana kubwa sana ndani yake. Kwanza ni kujali muda wake, tambua kwamba mtu huyu ameacha biashara nyingi akaja kwako hivyo ni muhimu sana kujali muda wake.
Onyesha kuwa karibu naye. Kama utashindwa kumweka karibu yako mteja lazima utampoteza. Kama kuna wenzako walifanya nae biashara na bado wanaendelea kuwa karibu nae atarudi kule wanapomleta karibu.
Kuna huduma zile ambazo mteja analipia kwanza kisha baada ya muda ndio kazi yake inakamilishwa. Hapa ndipo kuna matatizo mengi kama mteja amekuamini akakulipa pesa yake halafu anasubiria bidhaa yake unatakiwa uwe makini sana. Hii ndio sehemu ambayo mteja anaweza kufahamu vyema. Hii ndio sehemu ambayo inahitaji umakini kuliko zote.
Kuna wakati unaweza kusababisha mteja akuone wewe ni tapeli kwasababu tu unashindwa kuwa nae karibu. Sio sahihi kabisa mteja awe ndiye anaekutafuta mara kwa mara, kutomtafuta mteja na kumpa taarifa za kazi yake moja kwa moja atapata hisia za kutapeliwa kazi yake au uzembe mlio nao. Haijalishi umepata tatizo gani bado unatakiwa uwe karibu na mteja na aelewe vyema kila kianchoendelea.
Mteja ndio mtu wa muhimu sana kuliko hata biashara yako. Biashara yako inaweza kufa hata leo lakini kama ulikuwa na wateja wanaokuamini ukianza upya watakuwa na wewe.

 

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading