HATUA YA 133: Mafanikio Yanagusa Sehemu Hizi Tatu Muhimu.

jacobmushi
By jacobmushi
3 Min Read
Mojawapo ya Makosa wengi tunafanya ni kuweka nguvu sehemu moja ambayo ni kutafuta pesa halafu tukasahau sehemu nyingine za muhimu sana.
Kama utatumia nguvu zako zote kutafuta pesa  ukasahau afya yako, ukasahau mahusiano yako, ukaisahau roho yako hata ukipata pesa nyingi kiasi gani huwezi kufurahia.

 

Tukiweza kutengeneza uwiano mzuri katika kufanya kwa bidi itatuletea matokeo bora ambayo yanatuletea furaha kila kona ya Maisha yetu.
Afya.
Afya ni sehemu ya muhimu sana kwenye mafanikio yetu. Kama utakuwa mgonjwa hutaweza kutafuta pesa, hata kama tayari unazo hutaweza kuzifurahia zinaweza kuishia zote kwenye matibabu. Kama afya yako ni mbovu hutaweza kufurahia mahusiano yako. kuna ndoa nyingi zina matatizo makubwa kwasababu ya ugonjwa, mwanaume ana pesa na kila kitu kizuri lakini ana tatizo. Kuna magonjwa huwezi kuyatibu kwa wingi wa pesa ulizonazo.
Wakati huu unatafuta pesa kwa bidii ni muhimu sana kuzingatia afya yako. kula vizuri, fanya mazoezi kila siku. Nenda kafanya uangalizi wa afya yako mara kwa mara.
Soma: Hiki ndio Kitu cha Muhimu Kuliko Vyote
Mahusiano.
Mahusiano yako na mwenzi wako kama upo kwenye ndoa ni ya muhimu sana kuyatazama hata kama uko bize na kutafuta pesa au kusimamia biashara. Usiwe sababu ya maumivu kwa mwenzako kwa namna yeyote ile.
Unafikiri ni kwanini watu wengi wamekuwa na Maisha mazuri sana lakini ndani ya ndoa kunawaka moto? Walitumia muda wote kutafuta pesa wakasahau kuwa pamoja.
Kama bado hujaingia kwenye ndoa endelea kutengeneza mazingira na tabia ambazo zitakuja kukuwezesha ufurahie kile unachokitafuta.
Mahusiano yako na familia kwa ujumla, watoto, ndugu zako, jamii inayokuzunguka. Lazima ujue kwamba jamii inakuhitaji na inahitaji mchango wako kwa namna moja ama nyingine.
Ukipata vitu vyote vya thamani unavyovitafuta halafu ukakosa mtu wa kufurahia nae huwezi kusema una mafanikio.
Ukipata kila unachokitafuta halafu ukazingirwa na marafiki wanafiki pekee waliokuja kwako kwasababu una pesa huwezi kuwa na furaha. Tengeneza mahusiano bora wakati unaelekea kwenye safari yako ya kutimiza ndoto zako.
Roho Yako.
Sehemu hii ni ya muhimu sana kwababu ndio inakuwezesha wewe upate ulinzi na usiingiwe na tamaa. Kama utashindwa kutengeneza roho yako  lazima utaingiliwa na tamaa, uuaji, na roho nyingine mbaya.
Tengeneza mahusiano bora na Mungu wako. Kama unasali Sali kwa bidii. Tenga muda ambao unakutana na Mungu wako. Watu wengi wenye furaha kwenye vitu walivyovitafuta hawakumuacha Mungu wakati wanatafuta pesa.
Ukijisahahu ukaacha roho yako bila Mungu hapo ndipo Roho chafu zitakuingilia. Na ukiingiliwa na Roho chafu utashindwa kuwa mtu mwema kwa familia yako na kwenye jamii.

 

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading