HATUA YA 134: Wewe Ndiye Mwenye Ramani.

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read
Wewe ndie mwenye ramani ya Maisha yako. wewe ndiye kiongozi wa Maisha yako. usitembee kama mtu ambaye hajui anapokwenda wakati ramani umebeba mkononi mwako.

Usiogopeshwe na wanaokukatisha tamaa. Kuna nyakati utapita ambazo unaweza kudhani umepotea njia lakini bado usiamua kukata tamaa. Itazame ramani kisha urudi kwenye mstari.
Kazi yangu sio kukupa wewe ramani bali ni kukuwezesha kufikiri na namna ya kuitumia ramani. Ramani yangu ni tofauti kabisa na ya kwako. Kila mmoja ana njia yake anayopitia.
Wewe ndie mwenye ramani ya Maisha yako unatakiwa ukubali kuwa imara katika hali zote. Maisha yako ni wewe ndie utakuja kuhukumiwa kwa yale uliyoyatenda. Kama ulipoteza muda wako hapa duniani kuwaridhisha wengine ukasahau unapokwenda utakuja kujuta.
Simama imara misukosuko ipo mingi kila njia unayopitia. Kadiri unavyopitia misukosuko mingi ndivyo inaonyesha kwamba unakoelekea kuna thamani kubwa.

Ukiona hakuna anaepambana na wewe kukuzuia ujue hakuna cha thamani ulichobeba. Usiogope wanaokuzuia kule unakokwenda ni pa kubwa sana.
Umebeba vitu vya thamani sana ndani yako ndio maana kuna misukosuko ndani yako. mwindaji hawezi kupoteza muda wake kuwinda pori ambalo hana uhakika kama kuna Wanyama.
Kadiri misukosuko ilivyo mikubwa ndio ujue thamani ya ulichokibeba ni kubwa kiasi gani. Usikubali kushindwa utakuwa umekubali kunyang’anywa kile kilichopo ndani yako. Endelea kung’ang’ania aliekutuma yupo nyuma yako anakulinda.
Jipatie Nakala ya Kitabu cha Siri 7 za Kuwa Hai Leo, Wasiliana nami kwa 0654726668.
Jacob Mushi.
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668
jacobmushi.com.
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading