Kwenye jamii zinazotuzunguka mara nyingi utakutana na watu wanaotamani kuheshimika. Ukiachana na kuwa na pesa nyingi au kumiliki mali nyingi zipo njia ambazo unaweza kuzitumia zikakuwezesha kujijengea heshima.

Usimueleze Kila Mtu Shida Zako.
Mara nyingi mtu au watu wanaweza kukudharau sana hasa pale wanapokuwa wanazifahamu shida zako. Kama jana umegombana na mwenzi wako watu wote wa karibu yako unawaeleza watakudharau. Umepitia changamoto Fulani unamueleza kila mtu unajiweka kwenye hatari ya kudharaulika. Watu wanapokuona tu unaendelea na Maisha yako wanajenga heshima Fulani. Unapopata matatizo hakikisha una mtu mmoja au wawili ambao ni wazuri wa kuweka mambo kifuani na uwaeleze. Wakiwa ni watu wabaya nao wataanza kukudharau. Kumbuka sio kila tatizo ni la kumueleza mtu mengine tatua mwenyewe.
Usipatikane Kirahisi.
Kama wewe kila anaekuhitaji anakupata dharau hua zinaanza. Unajua kitu chochote kisichopatikana kirahisi kinakuwa na heshima yake. Kama umezoeleka kuonekana onekana hovyo n ahata pesa bado huna watu wanakuwa hawakuheshimu. Jijengee tabia ya kujitenga na kufanya mambo yako kisha unakuja kuibuka baada ya matokeo. Jitokeze kwenye mambo ya muhimu ambayo yanakufanya uongezeke thamani na kuifikia ndoto yako.

Usiwe Muwazi Kwa Kila Mtu.
Sio kila mtu ni wa kumueleza mambo yako. kuna mambo usipoyasema wakaja kuona matokeo ndio wanajua kwamba wewe sio mtu wa mchezo mchezo kama walivyokuwa wanakuchukulia. Kama kila mtu atajua mipango yako na unakokwenda inakuwa rahisi sana kudharaulika. Ni sawa na kuuza ramani yako kwa adui. Unapokuwa muwazi sana hutajua yupi ni adui yako. unapokuwa muwazi sana watu wanaokutakia mabaya wanapata nafasi ya kujua watakufanyaje ushindwe.
Usiwe Mwepesi Kujenga Urafiki Usio Na Kusudi Maalumu.
Sio kila unaekutana nae akakuchangamkia unamfanya awe rafiki yako. Wengine ni maadui wengine wametumwa. Unapokuwa na marafiki wengi unajijengea nafasi ya kupotea kirahisi. Kuna wakati unapata tatizo kwenye Maisha yako unashangaa kila mtu anajua matatizo yako kumbe ni kwasababu ya wingi wa marafiki zako. Kama urafiki hauna kusudi lolote maalumu kwenye kuitimiza ndoto yako basi ni bora ukaachana nao. Heshima yako itazidi kuongezeka kama watu wachache watakuwa na nafasi ya kukufahamu wewe vizuri, wengine wakiendelea kuona matendo na kusikia habari zako.
Hizi ni njia chache ambazo zinaweza kukusaidia kujijengea heshima kwenye jamii inayokuzunguka zifanyie kazi.
Jipatie Nakala ya Kitabu cha Siri 7 za Kuwa Hai Leo, Wasiliana nami kwa 0654726668.

Karibu sana.
Jacob Mushi.
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading