Katika Maisha yetu hapa duniani yapo mengi tunafanya ambayo yanakuwa msaada kwenye Maisha yetu kila siku. Bahati mbaya sana kuna mengine ya muhimu sana tunasahau na kujikuta tukihangaika bila kupata baadhi ya majibu.


Kama utashindwa kukua kiroho hata upate mali zote za ulimwengu huu utaishia kuwa mtu mwovu au mtu asiye na utulivu wa nafsi. Roho ndio kiini cha mambo yote yanayoendela kwenye ufahamu wetu. Kama utashindwa kuwa na tabia ya kuikuza roho yako kupitia mafundisho ya Imani unayoiamini utaishia kuwa mtu mwovu.
Kama lilivyo shamba ambalo limelimwa halijaoteshwa chochote ndivyo moyo unakuwa ulipozaliwa. Lakini kadiri unavyoendelea kuishi hapa duniani na kuona mambo mbalimbali ndivyo unavyoota magugu ya aina mbalimbali.
Visasi, chuki, uuaji,wivu tamaa mbaya yote haya yanaletwa na mioyo yetu kutokukua ua kuota kwa magugu. Hivyo ni kama mioyo yenye maovu ndani yake una vichaka.
Ukiweza kujiungamanisha na Imani yako ukapata nafasi ya kujifunza mambo mengi Zaidi kulingana na Imani yako utakuwa kiroho na utaona matokeo bora katika Maisha yako.

Roho yako inapokuwa na vichaka ndipo unaweza kuchukua maamuzi ya kumuua mtu mwingine, kuua wazazi ili upate mali.
Moyo wako unapopandwa mimea mizuri unakuwa faida kwa watu waliokuzunguka. Unakuwa baraka kwa kile unachokifanya. Upendo wako kwa wengine unaongezeka.
Rafiki yangu ni muhimu sana kutunza na kuikuza roho yako. kwenye vitabu vya Biblia kuna neno linasema “Linda Moyo wako kuliko vyote ulindavyo maana ndiko zitokako chemchem za uzima” kama ukishindwa kulinda moyo basi uovu ndio utaanza kutoka ndani ya ,moyo wako.
Jipatie Nakala ya Kitabu cha Siri 7 za Kuwa Hai Leo, Wasiliana nami kwa 0654726668.
Jacob Mushi.
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading