Maisha yanasonga mbele, siku zinasogea leo ni Tarehe 1 May 2017 unasonga mbele? Malengo yako yanatimia? Muda unasonga mbele inawezekana wewe umesimama. Mipango yako haikwendi mbele.
Ni muhimu sana kutambua vitu vya kukuwezesha wewe usonge mbele.

 

Wewe ni Nani
Ni lazima utambue wewe ni nani. Kama hujajitambua wewe ni nani basi unaishi Maisha ya kawaida sana ambayo binadamu wengi wanaishi. Tambua kusudi la wewe kuwepo duniani. Bila ya kusudi unaishi Maisha yasiyo na thamani.
Unakwenda Wapi
Unakwenda wapi na kusudi lako? Ni picha gani kubwa uliyonayo juu ya kusudi ulilobeba? Kama hujui ni wapi unakwenda huwezi kujua ni gharama kiasi gani unatakiwa kulipa. Huwezi kujua ni nguvu kiasi gani unahitaji ili uweze kufika unapokwenda. Ukweli ni kwamba kama hujui unapokwenda huwezi kuanza safari. Jua unapotaka kufika kwenye Maisha yako yote kwa ujumla, Afya, Mahusiano, Fedha, Biashara, Kazi na Kusudi lako.
Unahitaji Vitu Gani Ili Kufika
Huwezi kujua unahitaji kubeba maji kiasi gani kama hujui umbali wa safari unayokwenda. Huwezi kujua ni chakula kiasi gani ubebe kama hujajua unakokwenda ni muda gani utakuchukua kufika huko. Hakikisha leo umeweza kujikumbusha tena ni wapi unaelekea na ni vitu gani hasa unahitaji ili uweze kufika kirahisi. Maarifa, ujuzi, na vingine vingi. Mitandao ya kijamii imerahisisha mambo mengi sana ambayo tulikuwa tunaona ni magumu sana.
Kwa sasa ukitaka ulimwengu ufahamu unachofanya unaweza kutumia mitandao hii na ukafikia watu wengi sana ukiwa chumbani kwako umekaa na kifaa chenye mtandao wa internet.
Watu Gani Wakuambatana Nao.
Huhitaji kila mtu, chagua watu sahihi ambao watakuwezesha kufika kwenye safari yako. haijalishi umekosea mara ngapi katika kuchagua watu. Unayo nafasi ya kufanya maamuzi tena. Usikubali kukaa na watu ambao hawana wanachokushauri kwenye kile unachokifanya. Kama watu unaokaa nao wanaponda unachofanya ni bora uondoke maana wanakuwa wanayonya ile nguvu na hamasa iliyoko ndani yako.
Soma: Hakuna Kinachopatikana Kirahisi
Unawezaje Kugundua Fursa zilizokuzunguka.
Kuna fursa nyingi zimekuzunguka kama utashindwa kuzigundua na kuzifanyia kazi utatumia nguvu nyingi sana kufika. Iwezeshe akili yako ifikiri mara kwa mara juu ya vitu vilivyokuzunguka vinavyoweza kukusaidia wewe kutoka. Maisha yako yako mikononi mwako.
Beba majukumu yote ya Maisha yako. Wajibu wako Ni Kubadili Maisha yako.

 

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading