Watu wote waliouumiza moyo wako dawa yao sio wewe kuwaumiza tena. Huwezi kuuzima moto kwa kumwagia petrol kulipiza kisasi ni sawa na kumwagia petrol moto unaowaka.

Mtu yeyote ambaye ameuumiza moyo wako kwa namna yeyote ile unaweza kumlipa kwa kufanya mambo mawili ambayo yatakuwa ni faida kwako na kwake yeye mwenyewe.

Jambo la kwanza ambalo ni la muhimu sana ni wewe kuamua kuwasamehe. Ili uweze kusonga mbele kwenye ndoto zako lazima ukubali kuwasamehe wote waliokuumiza. Huwezi kufika juu kileleni cha mafanikio kama unashindwa kuwasamehe watu wachache tu ambao wamekuumiza hapa chini ulipo.

Kama hao unashidwa kuachilia msamaha basi inaonekana wewe ukiwa na nafasi kubwa ya juu utawaumiza sana watu waliokutesa na kukuumiza. Kwasababu hiyo moja kwa moja kila unapofanya mambo ili usonge mbele kuifikia ndoto yako unakuwa unashindwa.

Embu ambua kusamehe. Kusamehe ndio dawa ya matatizo mengi sana hapa duniani. Embu angalia watu wote wanaofanya maasi kama wangeamua kusamehe dunia ingekuwa sehemu salama sana kuishi.

Soma: Fungua Njia Hizi

Jambo la Pili ni kujifunza. Kama makossa yale yale yataendelea kujirudia kwenye Maisha yako basi hakuna unachojifunza. Kama umeshautambua udhaifu wako ni upi basi ni muhimu sana kuwa makini ili usirudie kuwa sababu ya wewe kuumia.

Kama utashindwa ni wapi unakosea huwezi kusonga mbele. Kama ni mahusiano utajikuta kila wakati unabadilisha tu watu kwasababu umeshindwa kusamehe na hujaweza kujifunza. Kama ulishindwa kujifunza ni wapi unapokosea basi utaendelea kufanya makossa kila wakati.

Usikubali kuwa mtumwa wa Vinyongo, Visasi na kutokujifunza. Mtu mwenye maono makubwa hawezi kutumia muda wake kuumia kwasababu ya watu wachache waliomuumiza anatumia muda mwingi kujifunza kwenda kule anakotaka kufika.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading