HATUA YA 139: Hukumu Inayoanzia Ndani.

jacobmushi
2 Min Read
Kabla watu hawajaona maovu yako ni vyema sana wewe mwenyewe ukaweza kujigundua ulipokosea na nafsi ikaanza kukusuta. Watu wengine hawana nguvu yeyote kubwa sana Zaidi ya nafsi yako kukusuta kutoka ndani kwa maovu uliyoyafanya.

Dhamiri yako ikikushtaki ndani kwa jambo lolote unalolifanya hatua ya kuchukua ni kuliacha kabla halijafika kwa watu wa nje.
Kama ulianza kushitakiwa ndani yako ukapuuzia ni ngumu sana watu wa nje kukwambia unakosea ukaelewa. Zaidi sana ni pale utakapoona madhara ya jambo lile.
Jambo lolote unalolifanya na roho yako imeanza kukushitaki hakuna binadamu mwingine atakaekubaliana na wewe. Tatizo kubwa lipo kwa watu ambao dhamiri zao zimekufa. Watu hawa lolote wanalofanya huwa ni sahihi ndani yao. Roho zao haziwasuti.
Njia rahisi ya kujisaidia kwenye jambo lolote unalofanya jiulize wewe ukifanyiwa utakubaliana nalo? Najua kuna mambo ya siri.  Lakini kama unafikiri kuna jambo unalolifanya kwa siri na halifai kuonekana hadharani hata siku ukiwa haupo duniani achana nalo mara moja.

Yaani kama kuna jambo unalolifanya gizani sasa hivi na unaona kabisa siku ukija kufa likijulikana ni aibu sana liache mara moja. Bahati mbaya unaweza usife utaumwa utazidiwa kitandani kuna mambo yataanza kuwa wazi.
Mara nyingi unapotaka kufanya jambo Fulani la hatari kunakuwa na sauti mbili ndani yako moja ikikutaza na nyingine ikikuruhusu. Kama utashindwa kujua ni sauti ipi sahihi unaweza unajikuta umefanya makossa.

Jambo lolote unalotaka kulifanya au kuwafanyia wengine jiweke wewe kwenye nafasi ya hao unaowafanyia kama utajisikia sawa kabisa kufanyiwa hivyo wewe au mtu wa karibu unaempenda sana endelea kulifanya.


Jipatie Nakala ya Kitabu cha Siri 7 za Kuwa Hai Leo, Wasiliana nami kwa 0654726668.
Jacob Mushi.
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668
jacobmushi.com.
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading