Kutamani usichokistahili kunakusababisha uingie kwenye mitego ambayo inaweza kusababisha maisha yako yaharibike.      

Chochote unachokiona kizuri mbele yako kama huwezi kukilipia gharama basi hukistahili. Anza kwa kulipa gharama ili ufurahie mwishoni.  

Wengi tunapenda kufurahia mwanzoni baadae tunakuja kujuta wakati wa kulipa gharama.   Unatamani ndoa nzuri anza kulipa gharama sasa hivi kabla hujaingia kwenye ndoa. Ukiingia bila kulipa gharama utakuja kuilipa huko mbeleni na bahati mbaya inaweza kukuumiza sana wakati unailipa.  

Soma: Chagua Kulipa Gharama sasa hivi au uje ulipe baadae  

Kutamani usichokistahili ndio chanzo cha maovu mengi sana duniani. Kunasababisha vitendo vya mauaji na wizi.  

Mwanadada anatamani mali na vitu vya anasa na hajalipa gharama ili astahili inambidi autoe mwili wake.   Kijana wa kiume anatamani Maisha mazuri lakini hataki kulipa gharama anajiingiza kwenye vitendo vya ujambaza na madawa ya kulevya.  

Ni kweli unastahili kupata vitu vyote vizuri unavyotamani lakini huwezi kuvipata bila ya kulipa gharama. Gharama zipo nyingi kama kufanya kazi kwa bidii, kutafuta maarifa ya kutosha, jichanganya na watu wenye fikra chanya.   Kuwa na maono makubwa yafanyie kazi hadi yatokee kuwa kweli. Kamwe usitegemee kupata unachokitamani Maishani mwako kwa njia halali bila ya kulipa gharama.

Rafiki yangu unaesoma Makala hizi kila siku endelea kulipa gharama hadi uifkie ile ndoto yako kubwa.      

Jacob Mushi. Entrepreneur & Author  

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading