Kuna tabia ambayo inawakumba watu wengi na inawafanya washindwe kufikia kule wanakotaka kwenda. Tabia ya kuishia njiani, mara nyingi huletwa na kukata tamaa au kuridhika na kile kizuri kidogo ulichoanza kupata.
Kukata tamaa.
 
Usikubali kukata tamaa au kukatishwa tamaa na wengine. Wewe ndio uliona picha kubwa ya unapoelekea. Usiogope changamoto unazokutana nazo njiani. Kama hakuna changamoto basi ujue unapoelekea hakuna thamani kubwa.
Umeanza ile biashara uliyokuwa unatamani kuwa nayo lakini unakaribia kuacha kwasababu ya hasara na changamoto unazopitia. Usikubali kuishia njiani maliza ulichokianza.
Soma: Usitazame nyuma
Umeanza mahusiano lakini sasa unataka tena kuishia njiani kwasababu ya changamoto unazokutana nazo. Huyo ulienae humuelewi elewi sawa lakini isiwe sababu yaw ewe kuishia njiani endelea kupambana. Utaitwaje mshindi kama hujaingia kwenye shindano? Hilo ndio shindano lako pambana hadi upate ushinde.
Kuridhika na Matokeo Kidogo.
Usikubali kabisa kulewa na matokeo madogo ambayo unayapata. Hii inaweza kuwa sababu ya wewe kujisahau na kuishia njiani. Kumbuka ile picha yako kubwa itazame mara kwa mara ili usije kujisahau na hizi picha ndogo ndogo ulizoanza kuzifikia.
Rafiki yangu wanaopewa medali ni wale pekee waliomaliza mwendo. Usikubali kuishia njiani usikubali kurudi nyuma.
Ndio mafanikio sio kitu kirahisi lakini pia kubakia hivyo ulivyo sio kitu kirahisi utateseka sana.
Endelea kusonga mbele hadi uifikie ndoto yako.

 

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading