HATUA YA 142: Wengine Wanafanyaje, Wewe Unafanyaje?

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read
Wakati mwingine lazima ujiulize maswali hasa pale unapofanya jambo moja linalofanana na wengine. Wenzako wanasonga mbele lakini wewe umebaki nyuma. Lazima ujiulize maswali ili uweze kusonga mbele.

Kwa kujiuliza maswali ndipo tunapata majibu ya matatizo yanayotusonga. Ndio sio vyema kujifananisha na wengine lakini pale inapotokea wenzako mlioanza pamoja wanasonga mbele na wewe umebaki pale pale lazima uanze kuangalia ni wapi unakosea.
Kama wenzako wametoka kwenye fani zao sio kwa bahati, ninaposema sio kwa bahati namaanisha kwamba, hawajalala tu kisha asubuhi wakiwa hawajui lolote wakapata hayo mafanikio unayoyaona. Kuna mambo wamefanya ndio maana unaona matokeo.

Bahati mbaya sana wakati mwingine yale mambo yanayoleta matokeo makubwa hayana kelele sana mbele za watu. Kama hayana kelele unaweza usijue ni kitu gani wanafanya wenzako unakuja kushtukia wameshafikia hatua Fulani wewe unabaki unashangaa.


Yale mambo yanayoleta matokeo makubwa ndio tunaita siri za mafanikio. Huwa hazionekani hadharani kila mtu aone unafanya nini. Sio uchawi wala sio bahati bali ni vitu ambavyo wengi wanaogopa kufanya.
Kaa chini chunguza wanafanyaje mbona wao wanasonga mbele wewe umekwama? Embu tafakari ni wapi unakosea? Angalia ni vitu gani huwa hufanyi vizuri? Ni mambo gani unaogopa kuyafanya? Kuna watu huwa unaogopa kuwaelezea kile unachokifanya? Au labda ukikutana na watu ambao wamefikia mafanikio makubwa unaogopa labda ulichonacho ni cha kawaida sana?
Jiulize maswali fanya uchunguzi ujue ni wapi unakosea. Lazima utoke hapo ulipo na wewe ufikie mafanikio.

Nikukumbushe tu rafiki yangu USIISHIE NJIANI, FANYA NAMNA YEYOTE UTOKE HAPO ULIPOKWAMA.
Jipatie Nakala ya Kitabu cha Siri 7 za Kuwa Hai Leo, Wasiliana nami kwa 0654726668.

Jacob Mushi.
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668

jacobmushi.com.
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading