Kuna misemo ambayo ni ya ajabu sana nilikuwa naona watu wakiizoea kuitumia kipindi Fulani. Ukweli ni kwamba misemo hii inaweza kuwa sababu moja wa shida kubwa ulizonazo sasa hivi. Sio kila msemo ni wa kuchukua na kufanyia kazi kama ulivyo lazima uangalie ni kwa namna gani unakuletea faida kwenye Maisha yako.

 

Tumia pesa ikuzoee ni  msemo mzuri kama utauchukulia kwa namna ambayo itakuletea matokeo bora kwenye Maisha yako. Kwa mfano wewe ukasema naitumia pesa yangu kwenye kuwekeza na kwenye biashara hadi pesa hii inizoee utakuwa umejijengea namna bora ya Maisha yako.
Ukiamua kuuchukua msemo huu kwa namna ambayo wengi wamekuwa wanamaanisha utaumia. Umepata pesa kidogo au nyingi kwa akili zako ukajua ukienda baa kuzinywa basi zitakuzoea utakuwa umepotea. Ukichukua pesa ukaenda kwenye anasa na starehe zozote unazozijua wewe ukafikiri zitakuzoea utakuwa umeumia.
Soma: Mifuko Iliyotoboka
Unaweza kuzitumia pesa zikakuzoea pea au ukakuzoea umaskini. Chagua namna ambayo unakwenda kuzitumia pesa wewe mwenyewe. Kila kilichopandwa kina matokeo hakuna pando ambalo halina mavuno. Wewe ukichukua pesa ukazipanda kwenye biashara utavuna faida. Ukichukua pesa ukazipanda kwenye starehe na anasa utavuna umaskini, magonjwa, watoto, na aibu mbalimbali kwenye Maisha yako.
Chagua kupanda sehemu sahihi, chagua kutumia sehemu sahihi. Watu pekee wasio na akili ndio hutumia pesa nyingi Zaidi kwenye starehe kuliko kwenye uwekezaji. Usikubali kuwa mmoja wao wa wasio na akili.
 

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading