HATUA YA 145: Matarijio ya wengine Vs Matarajio Yako..

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read
Kwenye vitu tunavyofanya kila siku kuna mambo mawili huwa yanatuendesha katika kufanya. Inawezekana wewe upo upande mmoja wapo lakini lazima uchague kitu ambacho kitakuletea faida kwenye unachofanya.
Matarajio yako na matarajio ya wengine ni vitu ambavyo vinatuongoza. Wewe unaongozwa na nini? Unaongozwa na matarajio ya wengine? Kama unaongozwa na matarajio yaw engine unakuwa ni mtumwa kwa kiasi Fulani kwasababu usipoweza kuwaridhisha wale wenye matarajio yao juu ya unachofanya unawaumiza.
Chochote unachokifanya watu wanakuwa na maoni na uashauri mbalimbali. Wengine watakwambia kwanini usingefanya hivi na vile. Lakini yote hayo ni kwasababu ya waonavyo wao. Unachotakiwa ni kuchukua ushauri na kuchambua yale yanayofaa na yanayokuwezesha wewe ufike kule unapoona.
Matarajio yako ndio yana nguvu kubwa sana kwasababu yanakupa hamasa Zaidi kuliko ya wengine. Japokuwa sio kila tunalotarajia hutokea lakini ni lazima kuongozwa na matarajio yetu.
SOMA: WEWE NI MSHINDI
 
Ongeza bidii tarajia ushindi tarajia matokeo makubwa sana. Wako ambao wanatarajio ushindwe, wanatarajie ukwame, wanatarajia urudi nyumbani lakini wewe tarajio kufanikiwa kwenye kila unalolifanya.
Maisha yako yapo mikononi mwako kile unachokiwaza na kukitamka ndio kinakuwa. Ukianza kujiona huwezi utashindwa.
Washangaze kwa matokeo makubwa Zaidi ya walivyotarajia. Washangaze kwa vitu vipya ambavyo unakuja navyo kila siku hadi waseme tulitaraji angefanya hivi lakini amekuja juu Zaidi.
USHINDI NI WAKO. USIISHIE NJIANI.

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading