Nilipokuwa shuleni mojawapo ya somo nilikuwa nalifanya vizuri ni somo la hesabu. Sasa kitu ambacho nilikuwa nakiona hasa kwenye maswali ya hesabu ni kwamba pale swali unapoliona ni rahisi sana kulitatua basi kuna uwezekano mkubwa ukawa umefanya makossa. Kama swali likiwa gumu sana ukapambana na ukapata majibu basi unakuwa na uhakika kiasi Fulani.

Mara zote maswali ambayo niliyaona ni marahisi nilikuwa nayakosa. Hii ni kwasababu swali likishakuwa rahisi basi hulipi tena umakini kama swali ambalo ni gumu.

Kwenye Maisha hivyo hivyo vitu virahisi siku zote havipewi umakini kama ambavyo tunavyovipa umakini vitu vigumu. Changamoto na matatizo ya aina mbalimbali tunayopitia yanatufanya tuweze kufaulu mtihani wa Maisha. Magumu tunayopitia yanatufanya tuweze kutumia akili kubwa Zaidi ya tuliyozoea kutumia. Kama tunatumia akili kubwa Zaidi basi tunapata nafasi ya kukua kwenye nafasi nyingine.
Usipendelee sana tambarare, unapopita kwenye tambarare usijisahau ukabaki hapo. Usiweke vibanda kwenye tambarare. Tatizo linakuja pale tunapoweka makao kwenye tambarare tukasahau kwamba tulikuwa tunasafiri.
Kuanzia leo tafuta vile vitu unavyoogopa kuvifanya anza kuvifanya. Haijalishi ni vigumu kiasi gani wewe endelea kupambana hapo ndipo kwenye njia. Dhahabu haipatikani kwenye udongo mlaini. Dhahabu ipo kwenye miamba wewe ukikimbia miamba umekimbia dhahabu.
Endelea kutatua mambo magumu yaliyokusonga. Kila zito unalotatua linakuwa ni rahisi kwako.
Jipatie Nakala ya Kitabu cha Siri 7 za Kuwa Hai Leo, Wasiliana nami kwa 0654726668.

Jacob Mushi.
Mwandishi, Mjasirimali na Mhamaishaji
Simu: +255 654 726 668
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com  
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading