HATUA YA 148: Jijengee Tabia ya Kumaliza.

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read
Kama utakuwa na mambo mengi uliyofanya na kuyaacha nusu nusu hapo unakaribisha uvivu. Kuchoka sana kunasababishwa na kazi nyingi unazofanya na kuziacha bila kuzimaliza. Mara zote unapata hamasa sana pale unapoanza jambo na kulimaliza.

Unajiona mshindi pale unapomaliza majukumu yako uliyojipangia. Kama utakosa tabia ya kuanza na kumaliza huwezi kufikia mafanikio kwenye mambo unayoyataka.
Watu wengi tuna tabia ya kuanza mambo vizuri lakini hatuna tabia ya kufika mwisho hadi kukamilisha kazi zetu. Mtu mwenye tabia za mafanikio anamaliza yale anayoyaanza. Haachi viporo vingi vya kazi zake.
Unajijengea mizigo mingi ambayo hutakuja kupata muda wa kuimalizia.
Njia rahisi ya kuweza kumaliza mambo yako ni kwa kuchagua kuanza na mambo yale magumu wakati wa asubuhi. Hii ni kwasababu wakati huo ndio unakuwa na nguvu ya kufikiri na kufanya kazi. Akili yako inakuwa na nguvu wakati wa asubuhi.
Usikubali kufanya mambo mengi ambayo hutaweza kumaliza hata mojawapo. Tabia ya kufanya mambo mengi na kutokuyamaliza unajijengea sifa mbaya kwa aliekupa kazi au kwako wewe mwenyewe.
Chagua mambo machache yafanyie kazi hadi mwisho. 
Kama una njaa ukiona chakula unaweza kupakua kingi sana lakini unajikuta huwezi kula hata nusu ukamaliza. Hivyo ndivyo ilivyo kwenye kazi. Ni bora uchukue majukumu kidogo uyafanye vizuri na kwa ufanisi yakiisha uongeze mengine kuliko kubeba mengi halafu humalizi hata moja.
Jipatie Nakala ya Kitabu cha Siri 7 za Kuwa Hai Leo, Wasiliana nami kwa 0654726668.
Jacob Mushi.
Mwandishi, Mjasirimali na Mhamaishaji
Simu: +255 654 726 668
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com  
jacobmushi.com.
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading