Unajihurumia sana ndio maana hupigi hatua yeyote ya mafanikio. Ni mara ngapi umejaribu kufanya kitu cha tofauti hadi mwili wako na akili yako ikapata uchovu ambao hujawahi kupitia? Baada kufanya hivyo lazima unafurahia lile ulilolifanya.

Unajihurumia husomi tena vitabu. Unatoa sababu za kukosa muda, lakini unasahau kwamba kutokusoma vitabu ni hasara yakow ewe mwenyewe. Shuleni ungesoma kwa kuogopa kufeli mtihani na huku unatakiwa usome vitabu kwa kuogopa kufeli kwenye kile unachokifanya.
Unajihurumia sana kwa sababu unalala sana. Embu jiulize mara ya mwisho ni lini ulijinyima usingizi? Ni lini ulijitoa kwa ajili ya lile jambo unalolitaka yaani ukakosa usingizi ili tu ulipate?
Unajihurumia sana hufanyi mazoezi kwa ajili ya afya.
Unajihurumia sana Hufanyi kwa utofauti kwenye biashara yako.
Unajihurumia sana ndio maana huoni tofauti kwenye hicho unachokifanya.
Amua kuumia kwa kiasi Fulani hadi utoke hiyo sehemu uliyozoea kukaa. Ili upande viwango vingine lazima ukubali kutoka hapo ulipokwama hapo ulipopazoea.
Lazima uwe tayari kulipia kile unachokitaka, iwe ni kwa kutoa jasho, kutoa pesa, kutoa muda na kadhalika. Bila ya kulipia gharama huwezi kutoka sehemu uliyokwama.
Usikubali kusimama sehemu moja muda mrefu wakati tupo safarini. Usinogewe na mazingiri ya tambarare ukasahau kuna mlima wa kupanda huko mbele. Furahia vya kutosha unapokuwa kwenye tambarare lakini usisahau kwamba mbele unaweza kukutana na bonde ama mlima hivyo jiandae pia.
#USIISHIE_NJIANI.
Jipatie Nakala ya Kitabu cha Siri 7 za Kuwa Hai Leo, Wasiliana nami kwa 0654726668.

Jacob Mushi.
Mwandishi, Mjasirimali na Mhamaishaji
Simu: +255 654 726 668
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com  
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading