Kufikiri na kutenda ni vitu viwili ambavyo huwa haviachana popote utakapofanya jambo. Mambo mengi mabaya na mazuri hua yanatokea hapa duniani kwasababu ya hivi vitu viwili. Ukitenda bila kufikiri utapata matokeo mabaya sana. Ukifikiri bila kutenda utabaki bila matokeo yeyote.
Haijalishi umefikiri vyema kiasi gani usipoweka kwenye matendo hakuna matokeo utakayopata. Kufikiri bila kutenda kunasababisha wengi kuishia kwenye maneno mengi sana bila matokeo.

Anza leo kufanyia kazi vitu hivi viwili kwa pamoja upate matokeo bora kwenye Maisha yako.

Embu jiulize ni mambo mangapi ulishafikiria kuyafanya na yakaishia kwenye mawazo peke yake?

Kosa kubwa ambalo unafanya ni kuishia kuwaza peke yake bila kupeleka kwenye matendo. Nenda hatua inayofuata ya vitendo kwamaana vitendo ndio vinaleta matokeo.

Embu jiulize ni mambo mangapi umeyafanya bila kufikri ukaishia kupata hasara na hadi sasa unajuta?

Kosa kubwa tunafanya ni kuingia kwenye biashara, mahusiano, na makubaliano ya aina mbalimbali bila kufikiri. Mwisho wa siku tunaishia kujuta na kulaumu vitu au biashara. Ukitafakari kwa undani unakuja kugundua ni mtu mwenyewe alifanya maamuzi bila ya kuishirikisha akili yake. Unaweza kumlaumu mtu kwa kukutapeli au kukudanganya biashara Fulani inalipa na wewe ukaweka pesa zako ukapata hasara kumbe ni wewe uliingia bila kufikiri. Ulichukua hatua bila ya kufikiri.

Tunapoelezwa jambo lolote zuri tukashirikisha akili zetu akili zetu hutupa maswali ya aina mbalimbali juu ya kitu kile kizuri. Maswali yale yanapaswa kuulizwa ili kupatiwa majibu. Na majibu ya maswali yale ndio hutupa nafasi ya kufanya maamuzi ya kuingia kwenye vitendo.

Kumbuka: Kufikiri na Kutenda kunakwenda pamoja siku zote.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading