Connect with us

HATUA YA 150: Jifunze Kusimama Mwenyewe.

HATUA ZA MAFANIKIO

HATUA YA 150: Jifunze Kusimama Mwenyewe.

Kuna nyakati utapitia kama hujajifunza kusimama mwenyewe utaanguka au utarudi kwenye hali uliyoizoea. Lazima ufikie sehemu ambayo utaanza kutembea na kusimama mwenyewe. Hii ni kwasababu kuna nyakati utapitia ni ngumu sana na utatazama kila upande utakosa msaada. Hata wale ulikuwa unawategemea sana watakaa mbali wakuangalie jinsi unavyoweza kufanya maamuzi mwenyewe. Kama hujajijengea tabia ya kuweza […]

Kuna nyakati utapitia kama hujajifunza kusimama mwenyewe utaanguka au utarudi kwenye hali uliyoizoea. Lazima ufikie sehemu ambayo utaanza kutembea na kusimama mwenyewe. Hii ni kwasababu kuna nyakati utapitia ni ngumu sana na utatazama kila upande utakosa msaada.

Hata wale ulikuwa unawategemea sana watakaa mbali wakuangalie jinsi unavyoweza kufanya maamuzi mwenyewe. Kama hujajijengea tabia ya kuweza kusimama utajikuta wewe mwenyewe unakuwa ni tegemezi kwa asilimia kubwa kwa wengine na kusababisha kuumia au kukata tamaa.

Jifunze kusimama mwenyewe hata kama watu watakataa kabisa mawazo yako. Hata kama watakwambia mawazo yako hayatakufikisha mbali endelea kusonga mbele kwasababu unakiamini kile unachokifanya.

Jifunze kusimama mwenyewe maana kuna nyakati watu hawatakufuata hadi waanze kuona mwangaza wa kule unakosema unakwenda. Ili ufikie viwango vya watu wengi kuwa nyuma ya kile unachokifanya lazima ukubali nyakati nyingine za kutembea na kusimama mwenyewe.

SOma: Ushindi Ni lazima Kwako

Usikubali kuacha au kurudi nyuma tu kwasababu kuna watu wamekuacha peke yako njiani. Ndoto yako ndio ikianza kuonekana ni kweli utaanza kuwaona wengi sana wakiwa nyuma yako.

Kusimama mwenyewe kunaiwezesha akili yako kufanya kazi vyema na kutatua changamoto kubwa Zaidi ya ulizozizoea. Kusimama mwenyewe kuna ujasiri na uzoefu wa kufanya mambo peke yako.

Kusimama mwenyewe kunaonyesha ni jinsi gani unaweza kuwa kiongozi bora.

JacoMushi.

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua Timiza Ndoto Yako

Pata vitabu vya biashara na mafanikio hapa www.jacobmushi.com/patavitabu

Jipatie Blog na Utengeneze Kipato www.jacobmushi.com/jipatieblog

Jiunge na Kundi Maalum la WhatsApp www.jacobmushi.com/whatsapp

Continue Reading
You may also like...

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in HATUA ZA MAFANIKIO

To Top