Jana katika matembezi yangu pembezoni mwa ziwa Victoria nilikutana na watu wakiogelea.

Kwasababu kule kwetu hatuna maziwa wala mito inayovutia kuogelewa nikasema ngoja niongeze uzoefu wangu kwenye maji ya ziwa hili la pekee.

Kutokana na mimi kutokujua kuogelea vizuri wale waliokuwa wakinitazama wakagundua mapema.

Wakaniambia maeneo haya kuna mamba sana,  kwa mtu kama wewe sio mzoefu ni rahisi sana kuliwa na mamba.

Moyo wangu ukaingiwa na hofu,  hamu ya kuogelea ikaniisha, baada ya habari ya kuliwa na mamba.

Kilichonifanya nisiogolee sio kutokujua kwangu vizuri bali ni hofu ya kuliwa na mamba.

Hofu ya kuliwa na mamba ikakaa kichwani mwangu hata nikienda sehemu isiyo na mamba naogelewa kwa woga na hofu ya kuliwa na mamba.

Kitu cha kujifunza hapa,  wakati unaanza kufanya biashara kuna watu walikueleza hadithi za waliopata hasara na kufunga biashara zao.
Wakati unaanza kuelezea ndoto yako kubwa jinsi utakavyoitimiza kuba watu wakakueleza ni jinsi gani utakutana na vikwazo.

Hayo waliyokueleza ni ya kweli lakini hayatakiwi yawe sababu ya wewe kushindwa kuanza.

Bahati mbaya sana wewe unawaza kuitumia hofu hizo kama sababu ya kushindwa.
Unabadili lengo lako kwasababu ya taarifa ulizopewa.

Kamwe usikubali hofu unazojazwa zikuzuie wewe kutimiza ndoto na malengo yako. Hata kama ni kweli mamba yupo lakini bado unaweza kuogelea. Kama kuna wengine wazoefu wanaogelea nenda katafute sehemu isiyo na mamba uongeze uzoefu wako kisha uje huku kwenye mamba.

Sehemu yenye kikwazo ndio sehemu yenye madini. Kama utaikimbia utakuwa umekimbia madini. Nenda katafute nguvu ya kukabiliana na kikwazo.

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading