HATUA YA 152: ULIITWA MAJINA YA WANYAMA?

jacobmushi
1 Min Read
Tulipokuwa wadogo mara nyingi tunapokosea wazazi wetu wengi walikuwa wanatuita majina ya wanyama.

Kulingana na tabia zako,  inawezekana ulishawahi kuitwa, kondoo, mbuzi, ng’ombe, mbwa,  na mengine mengi.

Lakini ni wachache sana waliotwa Simba au Tai pale walipofanya vizuri.

Majina ya wanyama hawa wadhaifu yanaweza kuwa sababu ya wewe kurudi nyuma kimaendeleo.

Pale unapoona ndoto yako halafu ukajisemesha mwenyewe “hivi nitaweza kweli? ”  ukikubali maneno kwamba hutaweza ni umekubali kuwa mmoja wapo wa maneno uliyonenewa.

Sifa ya wanyama hawa ni mbaya wapo kwa ajili ya kuliwa nyama,  wengine ni walinzi.

Wewe ni binadamu usikubali kuishi maisha kama ya mnyama. Una nafasi ya kufanya zaidi.

Usikubali kuondoka duniani ukiwa unamiliki nyumba ya kuishi peke yake. Hilo kila mtu anaweza.

Usikubali kuacha watoto tu huku duniani. Hilo kila kiumbe kina uwezo wa kuzaliana.

Tumia ubinadamu wako kufanya makubwa.

Kuna watu walifeli darasani sio kwasababu hawakuwa na uwezo ila ni kwakuwa waliambiwa wewe ni kondoo pale walipofanya makosa nyumbani.

#USIKUBALI MANENO ULIYONENEWA YAWE SABABU YA KUSHINDWA KWAKO.

#USIISHIE_NJIANI

Jacob Mushi
Mwandishi, Mjasiriamali na Mhamasishaji
Simu: 0654726668
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com
Blogu: www.jacobmushi.com

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading