HATUA YA 153: USIWALAZIMISHE WAKUELEWE

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read
Moja ya makossa ambayo wengi wetu tunafanya ni kuwalazimisha baadhi ya watu Fulani watuelewe kwenye vile vitu tulivyochagua kufanya. Sasa changamoto inakuja pale ambapo unatarajia watu Fulani wakubali kile unachokifanya halafu wakakaa kimya kama vile hawakuoni.

Kama mategemeo yako yalikuwa ni watu Fulani Fulani wakukubali badala yake wakakaa kimya unapata shida ndani ya moyo wako. Unachotakiwa uelewe hapo ni kwamba binadamu hatufanani hata yule mtu maarufu kuliko wote duniani ambaye kazi zake zinapendwa na watu wengi Zaidi bado kuna ambao hawamkubali hata kidogo.
Badala ya kupoteza muda wako kuwalazimisha baadhi ya watu wakuelewe wewe endelea kupiga kazi. Endelea kupambana kuna watu watajitokeza mbele ya safari. Wapo wengi sana na usio watarajia wataanza kuona kazi unayoifanya.
Kama wewe ni mwimbaji usikate tamaa pale ulipokuwa unajaribu kujipendekeza sehemu ukakataliwa.
Kama wewe ni muigizaji ulijaribu kujipendekeza kwa mtu maarufu Fulani hivi ili upate hata nafasi ya kuigiza kama mlinzi bahati mbaya akakutolea nje usigope kabisa.
Wewe ni mfanyabiashara umetoa bidhaa yako mpya ukiwa na hamasa kubwa umeipeleka ofisi Fulani ya tajiri mmoja hivi ili angalau aone upate sapote yake lakini akakukataa usiogope.
Yote hayo yanatokea kila mahali ukiona umekataliwa tumia hiyo kama hamasa ya kufanya kwa ubora Zaidi hadi wakutafute wenyewe. Endelea kusonga mbele milango mingine itafunguka huko mbele.
Hata wale usiotarajia kabisa kama wangekukubali watatokea na kusema nataka tufanye kazi pamoja. Mfungua milango ni Mungu mwenyewe hiyo milango iliyogoma kufunguka ulikuwa unajaribu kufuungua mwenyewe.
Endelea kusonga mbele usiishie njiani. Ongeza ubora fanya kwa bidi ipo siku usio itarajia milango yako itafunguka wale waliokutolea nje wataangalia pembeni wakiokuona unapita.
#USIISHIE_NJIANI.
Jipatie Nakala ya Kitabu cha Siri 7 za Kuwa Hai Leo, Wasiliana nami kwa 0654726668.

Jacob Mushi.
Mwandishi, Mjasirimali na Mhamaishaji
Simu: +255 654 726 668
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com  
jacobmushi.com.
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading