HATUA YA 155: Mbegu Yako Unapanda Wapi?.

jacobmushi
2 Min Read
Mbegu ndio chanzo cha matokeo ya vitu mbalimbali kwenye dunia hii. Kila mtu ana mbegu ndani yake. Iwe mbegu njema au mbegu ovu, kila binadamu ana mbegu kwa ajili ya matokeo mbalimbali ndani ya Maisha yake.

Kwa matokeo yeyote unayoyataka lazima ujue kupanda mbegu ulizonazo. Na sio kupanda pekee lazima ujue sehemu sahihi ya kupanda mbegu ili upate matokeo sahihi. Sio kila udongo hufaa kupanda nyanya. Ukipanda nyanya kwenye udongo wa kupandia mahindi hautapata mavuno sawa sawa.
Inawezekana wewe unalalamika hupati matokeo unayoyataka kumbe sababu ni kule unapopanda mbegu zako. Hakikisha unatambua mbegu uliyonayo, hakikisha unafahamu sehemu sahihi ya kupanda mbegu yako.
Mbegu isipopandwa haiwezi kuleta matokeo yeyote. Mbegu haijipandi yenyewe lazima utoke uende shambani ukaandae shambani kisha uweke mbegu chini. Wako wengi wanalalamika  kuhusu Maisha yao kumbe hakuna sehemu yeyote aliyopanda mbegu.
Usiishie kusema ipo siku Maisha yatabadilika wakati hakuna mbegu unayopanda. Panda mbegu kwa watu unakutana nao kila siku. Unakutana na watu wapya unawaachia mbegu gani ndani yao? Unawaachaje? Wanaondoka wakifikiri wewe ni mtu wa namna gani? Je wanatamani kufanya kazi na wewe?

Tunapanda mbegu kwa watu, mbegu zilizopo ndani yetu tunazipanda kwenye Maisha ya wengine. Ni muhimu sana kujua sehemu sahihi unayopanda mbegu yako ili ujue unasubiria matokeo gani. Kama utapanda mbegu kwenye miamba au miiba utasubiria sana mbegu zako kuota.
Lazima ufahamu kwamba wakati mwingine shamba linaandaliwa linafyekwa miiba na kulimwa. Hivyo kama ni watu lazima ujue unawaandaa vipi ili wapokee mbegu kwenye shamba ambalo ni safi. Ukipanda mbegu kwao bila kuwaandaa lazima matokeo yatakuwa madogo.
Jipatie Nakala ya Kitabu cha Siri 7 za Kuwa Hai Leo, Wasiliana nami kwa 0654726668.

Jacob Mushi.
Mwandishi, Mjasirimali na Mhamaishaji
Simu: +255 654 726 668
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com  
jacobmushi.com.
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading