Picha ya maisha yako iliyoko vichwani mwao ni maisha yako yaliyopita.
Wanakumbuka zaidi mambo ambayo ulishayafanya siku kadhaa zilizopita.

Wanakumbuka hali ya umaskini waliokuwa wanaouona kwenye maisha yako.
Wanakumbuka vile walivyokuzoea ukiongea.

Wanakumbuka  tabia zako za awali.

Bahati mbaya sana wanasahau kwamba inawezekana leo umeanza kubadilika.
Kama wewe hutajua kwamba hawa watu hawajajua unachoendelea kufanya sasa hivi unaweza kukatishwa tamaa na maneno yao.

Kamwe usikubali maneno yao yakupe hofu kwenye safari uliyoianza.
Watasema huyu si tunamfahamu?  Anasema ameanza biashara?  Huyu si alifeli kidato cha nne?

Huyu kwao si maskini kabisa huyu? Hatafika mbali tunamfahamu!

Haya maneno usikubali yakurudishe nyuma,  hawa watu wanaifahamu tu historia yako hawajui kama umebadilika.

Hawajui kama umeshaanza kusoma vitabu.
Hawajui kama umekutana na watu wenye mtazamo chanya kuliko wao.

Hawajui kama tayari una ndoto kubwa kuliko wao wanavyowaza.
Hawajui kama na wewe una malengo ya maisha yako tena makubwa sana na unayafanyia kazi.

Kwasababu hiyo wewe endelea kukazana usikubali tafsiri za zamani juu ya maisha yako zikurudishe nyuma.

Endelea kusonga mbele hadi waanze kufuta tafsiri za zamani juu yako.

Hali yeyote mbaya sio ya kwako ila ukiamua kubaki nayo itakuwa yako.
Kataa kurudishwa nyuma kwa maneno ya watu juu yako.

#USIISHIE_NJIANI

Jipatie nakala yako ya kitabu Siri 7 za Kuwa Hai Leo. Wasiliana nami kwa 0654726668.

Jacob Mushi.
Mwandishi, Mjasiriamali na Mhamasishaji.
Simu: +255 654 726 668
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com
jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading