Wakati unafanya maamuzi ulikuwa mwenyewe, wakati unaamua kupambana kwa namna yeyote ili utimize ndoto yako ulikuwa na watu wachache sana. Lakini sasa hivi unavyoanza kutembea kuelekea kwenye kuitimiza utakutana na maoni ya watu wengi sana juu ya kile unachokifanya.
Usisahau kwamba bado dunia haijabadilika. Bado watu waovu wapo hivyo usishangazwe na watu watakaokwambia wewe huwezi. Kuna wakati utashangaa hivi hawa watu walikuwa wapi wasikushauri wakati unaanza?
Walikuwa wapi wakati unapitia magumu hujui pa kwenda hujui cha kufanya, wakati unatamani kujiua kwasababu ya mateso uliyokuwa unapitia hakuna aliekuwa anakuona. Cha ajabu sasa hivi umeanza tu safari ya kutimiza ile picha kubwa ndani yako wanaanza kuja kukushauri cha kufanya.
Inawezekana ukashangaa san ahata usio watarajia wakawa kinyume na wewe. Anaweza kuwa mtu wako wa karibu sana uliekuwa unamuamini sana akaanza kukukatisha tamaa. Usikubali kabisa wapotezee.
Hakuna namna nyingine ya kuepuka kelele ambazo zipo njiani Zaidi ya kuendelea kutazama kile ambacho kinakufanya ufanye.
Nilikutana na mtu mmoja akaniambia Jacob unapoteza muda na hizo Makala unazoandika. Nikamtazama nikasikitika kwasababu hajui hata historia ya maisha yangu. Hajui kama kuna siku nilikata tamaa ya maisha nikachukua kisu nataka kujiua nikakutana na mtu akanitia moyo. Hajui kabisa kuna nyakati nilikuwa sina mwelekeo wa maisha yangu leo tu anatokea tu anasema ninapoteza muda. Maana yake ni kwamba anataka nirudi kule nilipokuwa.
Ukikutana na kelele za kukuzuia kwenye safari yako ndugu yangu itazame sababu yaw ewe kufanya kile unachokifanya. Embu jione wakati ule ukiwa huelewi pa kwenda halafu jiambie ni kweli huyu mtu anataka nirudi pale? Kisha msamehe kwasababu hajui ulipotoka. Endelea na safari.

 

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading