Usiparamie mti wakati shoka ni butu. Utatumia nguvu kubwa sana lakini utapata matokeo madogo.
Abraham Lincoln aliwahi kusema kwamba akipewa masaa sita kukata mti atatumia masaa manne kunoa shoka lake. Hii inatufundisha kwamba ni muhimu sana kujiandaa vyema kwa kile unachotaka kufanya.
Hii haimaanishi kwamba uchelewe kuanza kwa kisingizio unanoa shoka. Au unajiandaa. Chochote unachotaka kufanya maandalizi ni muhimu sana.
Wanajeshi pia hawafanyii mazoezi vitani. Ukisema unakwenda kujifunzia vita vitani lazima adui akushinde.
Nataka kukwambia hivi Noa shoka lako kila siku kwani kuna pambano mbele yako linakuja. Noa shoka lako kila unapomaliza jambo moja.
Unapovuka changamoto moja tambua kwamba inayofuata itakua ni kubwa Zaidi hivyo ni muhimu kuendelea kunoa shoka.
Kunoa shoka ni kujiweka bora kwa ajili ya mapambano ya kuifikia ndoto yako. Changamoto ni nyingi sana kama hutajiandaa kwa kunoa shoka kila kitakachokuja mbele yako utakikimbia.
Sitaki kukudanganya kwamba pambano litakwenda kuwa rahisi. Nenda vitani ukitambua kwamba unakwenda kupigana na mtu aliejiandaa vyema. Hivyo ni muhimu sana na wewe uwe umejinoa sawasawa.
Kumbuka: Haukwendi kupambana na mtu. Usijiandae kwenda kupambana na mtu yeyote. Jiandae kwenda kupambana na changamoto. Jiandae kwenda kupambana na ushindani kwenye biashara yako na wala sio watu. Jiandae na uwe Bora zaidi ili kushinda kila kinachokuja mbele yako.
Karibu sana.
Tunakwenda kunoa Shoka pamoja katika mtandao huu.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
Email: jacob@jacobmushi.com
Blogs: www.jacobmushi.com,  www.jacobmushi.com

jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading