HATUA YA 160: Mtu Huyu Kaa Nae Mbali..

jacobmushi
2 Min Read
Tunazungukwa na watu wengi sana katika kazi zetu na maisha yetu ya kila siku. Kuna baadhi ya watu ni sumu ya mafanikio yetu. Wanakuwa sumu kwa maneno wanayosema kwetu, kwa vitendo wanavyotufanyia. Kuna aina ya watu ambao ukiwa unafanya nae kazi akafanya makossa yeye yupo tayari afanye namna yeyote ile ili wewe uonekane umekosea. Mtu huyu kaa nae mbali.
Kuna mtu ambaye yeye hakubaligi kushindwa hata siku moja. Kama mmekuwa mnabishania jambo Fulani anataka yeye aonekane anajua vingi kuliko wengine. (Usikae katikati ya wabishanao) mtu wa aina hii yupo tayari kuona wewe unaaibika ili yeye aonekane shujaa. Kaa nae mbali.
Mtu ambaye yupo tayari kuona wewe unashindwa ili yeye ashinde kaa nae mbali.
Mtu ambaye yupo na wewe kwasababu ameona atapata faida Fulani kisha aondoke zake huyu kaa nae kwa makini. Kuna watu wako tayari kukunyonya hadi unafilisika kisha wanakukimbia na kuanza kukusema. Hujaona marafiki ambao wakati pesa ikiwepo wapo pamoja wanakula zikiisha anakimbiwa na wale walikuwa wanakula nae ndio wanakuja kumsema Fulani yupo hivi na hivi. Kaa nao mbali watu wa aina hii na Zaidi acha starehe.
Mtu ambaye wewe ukimhitaji hayupo tayari kuja, iwe ni kwenye kazi au matatizo. Lakini yeye akikuhitaji analazimisha kabisa utokee. Usipotokea anaanza kukulaumu. Watu wa aina hii tunawaita wabinafsi wanataka kusaidiwa lakini hawataki kuwasaidia wengine. Ndio ni kweli humsaidii mtu ilia je kukusaidia tena lakini kama ni mtu wa karibu na hajali muda wako wewe lakini anataka yeye ujali wa kwake huyu kaa nae mbali.
Kwa neno rahisi unatakiwa uweze kuyamiliki maisha yako mwenyewe uwe una uwezo wa kufanya maamuzi yako bila kuingiliwa.

Rafiki Yako,

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/coach

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading