“Kama Sio Mimi Kumsaidia Asingefika Pale” Inawezekana umeshakutana na kauli hii mahali au ni wewe ulishaitamka. Embu itafakari uone ni kwa namna gani inaweza kuwa chanzo cha watu kutofanikiwa? Kwanza tunamuona mtu mmoja anaesema kwamba alimsaidia mtu akafikia hatua Fulani. Pili kuna huyu anaesemwa kwamba amesaidia na watatu ni huyu anaeelezwa na mwenzake.    

Inawezwekana wewe ulishakuwa upande mmoja kati ya hizo hapo tatu. Labda ni watu walikusaidia kipindi cha nyuma ukaweza kufanikiwa kimasomo na sasa wanasema kila mahali kwamba wao ndio chanzo cha mafanikio yako. ni kweli inawezekana wamehusika kukusaidia lakini kwa kawaida kama binadamu unampomsaidia mtu sahau.    

Tunajifunza kwamba tunapowasaidia wengine tusitegemee chochote kutoka kwao. Tunaposema chochote tunamaanisha chochote, kuanzia heshima, asante, au kurudishiwa fadhila yeyote. Haijalishi ulimsaidia mtu kiasi gani hata kama amekudharau wewe kaa kimya tu hakuna haja ya kuanza kusema “huyu nilimsaidia sana sasa hivi amefanikiwa ananidharau”.    

Unapokaa kimya unamtengenezea nafasi yay eye kuja kutubu kwako endapo anayofanya sio sahihi. Wako wengine hulalamika kwasababu walitegemea kijana wa watu wamemsaidia basi akishapata kazi wataanza kuona matunda ya kazi yake. Bahati mbaya sana maisha yamekuwa magumu Zaidi kuliko walivyofikiri. Kijana wa watu inambidi akae kimya tu maana hana cha kupeleka. Kukaa kimya unaonekana una dharau.    

Ni vyema sana kutoa msaada na kusahau kabisa. Unaposahau unamruhusu Mungu afungue milango mingine ya Baraka kwako. Kama wewe ulimpa huyu Mungu atamgusa mwingine aje akupe wewe. Hivyo toa na sahau kabisa. Unapolalamika unasababisha hata yule uliemsaidia mambo yake yasiende vizuri kwasababu ya maneno yako.

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading