HATUA YA 162: Huyu Ndio mtu Maskini Kuliko Wote Duniani..

jacobmushi
2 Min Read

Umaskini sio kukosa vitu, Umaskini ni kubaki na vitu vilivyopo ndani yako bila kuvitoa kwenye dunia hii. Mtu pekee aliekufa masikini ni yule alieondoka na vitu alivyozaliwa navyo. Yule aliendoka bila ya kufanya chochote hapa duniani juu ya kusudi la Mungu lililopo ndani yake.
Ni kweli huwezi kutoa ambacho huna lakini kila mmoja ana kitu cha kutoa kilichofichwa ndani yake. Ni jukumu lako kugundua kile kilichoko ndani yako ili usiendelee kuishi maisha ya kimasikini.
Mtu yeyote mwenye mali ambazo amezipata kwa halali alitoa kitu ndani yako ndio akapata. Wengine wametoa nguvu zao wakafanya kazi za watu kwa bidii hadi wakapata mafanikio yao. Wengine walitoa akili na vipaji Mungu alivyoweka ndani yao ndio maana wakafikia mafanikio makubwa unayoyaona.
Kukishikilia kile ulichonacho bila ya kukitoa nje unajiandaa kuwa maskini. Haijalishi ni sababu gani inakuzuia kutoa hiyo zawadi iliyopo ndani yako bado utakufa maskini.
Usikubali kuondoka duniani na vitu ulivyokuja navyo. Unayo kila nafasi ya kutoa kwenye jamii iliyokuzunguka. Maisha haya ni mazuri sana kama tutaweza kutoa kwa wingi kile kilichopo ndani yetu.
Utajiri upo ndani yako kama utaamua kutumia vile ulivyozaliwa navyo. Una kila sababu ya kufanikiwa. Una kila nafasi ya kufikia mahali unataka. Anzia hapo hapo ulipo, anza na kilichopo ndani yako.

Kamwe #USIISHIE NJIANI.

Usiache Kujipatia nakala ya kitabu Cha SIRI 7 ZA KUWA HAI LEO. Wasiliana name kwa 0654726668.
Jacob Mushi
Kufanikiwa ni Kuamua.
Mwandishi Mhamasishaji na Mjasiriamali.
Phone: +255654726668
jacobmushi.com.
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading