Marafiki waliokuzunguka wana mchango mkubwa kwako katika kukuangusha au kukufanya usimame. Hii ni kutokana na muda mwingi mnapokuwa pamoja lazima muwe mnazungumza. Sasa swali linakuja hapa mncahokizungumza ni nini? Inawezekana unafurahia kampani nzuri ya marafiki zako lakini kumbe yale ambayo mnajadili mara kwa mara yanasababisha Maisha yako yakwame.
Mnazungumzia Maisha watu?
Kama muda mwingi mnakuwa mnajadili Maisha ya wengine, iwe ni kwa ubaya au uzuri lakini inaweza kuwa sababu ya kupoteza muda na kusahau Maisha yenu. Kuna watu ambao msanii Fulani akinunua gari mpya au nyumba mpya lazima wajue.  Kila kinachoendelea duniani yeye anakijua, ukitaka taarifa mpya unaenda kwake.  Maisha yako yatakuwa hatarini.
Mnalalamika juu ya Hali Ngumu ya Uchumi?
Kama marafiki zako mkikaa mnatumia muda mwingi kuzungumzia hali ya uchumi kwa namna ya kulalamika badala ya kuzungumzia nini cha kufanya mnapoteza muda. Huo muda mngetakiwa mjadili njia za kufanya uchumi wenu uwe mzuri.
Soma: Hawa ndio Watu wa Kukaa nao Mbali
Mnazungumzia Namna ya Kupata Suluhisho la Changamoto zenu?
Marafiki ambao unatakiwa kuwa nao ni wale ambao wanapenda kuzungumzia suluhisho la changamoto mbalimbali ambazo mnapitia na sio kulalamika. Tafuta watu ambao ukikaa nao wewe unakua na unajifunza kwa kupitia wanayofanya na kuongea.
Mnazungumzia Namna ya Kuboresha Maisha yenu?
Tafuta marafiki ambao muda mwingi wanazungumzia maendeleo. Wanazungumzia kutoka sehemu moja waliyopo waende mbele Zaidi. Kwenye masomo au biashara wanazofanya wanazungumzia Zaidi juu ya kusonga mbele. Hawa ndio marafiki wanaokufaa.
Mnazungumzia Namna ya Kupata mawazo Mapya?
Marafiki zako ukikaa nao unapata mawazo mapya juu ya kile unachokifanya?  Unapata mawazo mapya ya kubadilisha Maisha yako? Kama jibu ni ndio basi upo na marafiki ambao wanakufaa.
Kumbuka:
Unatakiwa uchague marafiki ambao wanafanya kitu ambacho kinafanana na unachokifanya. Ndege wanaofanana huruka pamoja.
Unatakiwa uwe na marafiki wachache ambao mnalingana vitu, maendeleo pamoja na uwezo wenu wa akili. Ongeza marafiki ambao unajifunza Zaidi kwao, ongeza marafiki ambao wamekuzidi kimaendeleo na kwenye kile unachokifanya, hapa lazima utaweza kusogea mbele.

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading