Wanadamu wote Tuna muda sawa ambao ni masaa 24 kila siku.  Yaani kila mmoja ana mchana na usiku. Hakuna ambaye muda wake umepunjwa.  Kinachofanya mtu aonekane ana muda mwingi na mwingine hana ni vipaumbele vyetu.

Sasa kwenye vipaumbele ndio kunaleta tofauti ya mambo na watu waliofanikiwa. Watu waliofanikiwa wanajua namna ya kupangilia muda wao vizuri ndio maana umewaletea mafanikio.

Ni muhimu sana kujiuliza muda wako unautumiaje kila siku.  Ni vitu gani vinachukua muda wako zaidi kwani hivi ndio vinaweza kukuletea utajiri ama umaskini.

Kama muda wako mwingi unautumia kufanya mambo yasiyo na uzalishaji au mchango wowote kwenye ndoto zako Utachukua muda mrefu sana kuzifikia.
Muda tulionao ni mdogo sana na mambo ya kufanya ni mengi.

Hasa kipindi hiki ambacho mitandao imekuwa na nguvu kubwa sana kwenye maisha yetu,  watu wasio na vipaumbele muda wao mwingi umetekwa humo.

Lazima ujue ni vitu gani unafanya kwenye mitandao hii. Usitumie muda wako bure kufuatilia vitu ambavyo havina mchango kwenye ndoto zako.

Badala ya kupoteza muda kufuatilia maisha ya wengine tumia muda huo kuonyesha kile unachokifanya kwenye mitandao hii.

Tumia muda mwingi kujifunza na kukuza jina lako.

Marafiki unaowapa muda wako mwingi je wanaustahilii? Makala iliyopita nimekuuliza ukikaa na Rafiki zako mnaongea nini?
Wewe hapo utakuwa umejijibu kama wanastahili muda mwingi zaidi ni kina nani.

Muda ndio bidhaa ya pekee iliyobaki isiyobadilishwa. Tukiweza kuutumia muda wetu vizuri tutayafikia mafanikio makubwa.

#USIISHIE NJIANI

Jacob Mushi
Mwandishi, Mjasiriamali na Mhamasishaji.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading