HATUA YA 165: USISUBIRI MACHUNGWA CHINI YA MTI WA MNAZI

jacobmushi
2 Min Read

Mafanikio yako ni kama unavyotesha mti wa Mwembe au unavyopanda mahindi.
Mwembe Unachukua muda mrefu sana zaidi ya miaka kadhaa  hadi uanze kutoa matunda yake (sio hii ya kisasa)
Muda wote huo mwembe utahitaji huduma mbalimbali kama kunyeshea, mbolea,  madawa na vingine vingi.
Lakini wakati huo hakuna faida yeyote unaona kwenye mwembe,  unaweza kusubiri miaka kadhaa unauhudumia mwembe tu bila ya matunda yeyote lakini sasa ukianza kutoa matunda utaendelea hivyo muda mrefu sana.

Lakini tukija kwenye mahindi, ambayo yanaoteshwa baada ya miezi mitatu au minne watu wanakula mahindi.  Mahindi haya hayadumu,  ukishavuna huwezi kuja kuvuna mara ya pili.
Ukitaka kuvuna tena inakubidi uje uoteshe tena mahindi.

Katika maisha vitu vinavyodumu ni vile ambavyo vinachukua muda mrefu kwenye mwanzo.  Kama unaanza biashara unategemea faida baada tu ya kuanza hautadumu sana.

Kuna nyakati hasara kubwa unaweza kuzipata, lakini kwasababu unachokipigania unakijua hutaweza kukata tamaa,  hutaishia njiani.  Kama unaingia kwenye biashara kwa lengo la kupiga hela za haraka haraka utakuwa unafanana kilimo cha mahindi. Ukishavuna unasubiri tena kipindi kingine uanze kulima.

Kama unaona miezi mitatu mbele huwezi kuotesha mwembe,  utaotesha mahindi. Wengi wanaolalamika na kukata tamaa walikuja kwenye biashara wakiwa wanaona miezi michache mbele halafu wamepanda miembe.

Angalia maono yako na hicho ukichokipanda yanaendana? Inawezekana unakata tamaa kwasababu ulipanda mwembe ukifikiri unapata matokeo haraka.

Kama umeamua kuingia kwenye biashara au chochote unachokifanya anza kuwa na maono. Angalia kile unachokifanya kitakufikisha wapi kwenye maono yako. Hii itakusaidia usije kuwa unapoteza muda.

#USIISHIE NJIANI

Usiache kusoma Kitabu cha Siri 7 za kuwa hai leo wasiliana nami kwa 0654726668.

Jacob Mushi
Mwandishi, Mjasiriamali na Mhamasishaji.
Simu: 0654726668
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading