Tabia ya uvumilivu tunajifunza kwamba ndio inaleta Mafaniko, hasa pale tunapopitia changamoto.
Swala gumu linakuja pale unapowavumilia watu ambao ulifanya makubaliano nao yeyote yale. Hapa uvumilivu unaweza kuwa mgumu sana kwasababu unaemvumilia hajali wakati mwingine.
Tuseme unaemvumilia ni mtu uliemkopesha pesa. Mtu huyu kila wakati anakupa ahadi za nitakupa nitakupa, uvumilivu wa hapa unaweza kuwa mgumu sana. Kuna wakati inakubidi ufanye maamuzi ya kuchukua hatua nyingine ya ziada, labda kuachana nae au kwenda mbele zaidi.
Nimeandika makala hii kwa kukulenga wewe ambaye unavumiliwa na watu wa aina hii niliyoelezea hapo juu. Hakikisha unafahamu na kujali kile ambacho mtu amekupa. Kama mtu ameamua kuvumilia tabia yako na hubadiliki ujue kuna mwisho wake.
Kama mtu ameamua kuvumilia ahadi unazompa kila wakati halafu utekelezi ipo siku ataondoka. Hakikisha unathamini uvumilivu wa wale waliokuvumilia.
Ikifika nyakati mtu anasema uvumilivu umemshinda ujue umeshamuumiza na wakati mwingine kumharibia mambo yake mengi.
Heshimu sana maumivu unayowapa watu wanaokuvumilia. Wakati mwingine jaribu kushuka chini na kuomba samahani kwa yale unayoyafanya.
Mtu akishindwa kukuvumilia hawezi akaendelea kukuamini tena. Kile alichofanya na wewe hawezi kurudia tena.
Ili kulinda uaminifu wako na wengine jali yale wanayovumilia kwako.
#USIISHIE NJIANI
Usiache kusoma Kitabu cha Siri 7 za kuwa hai leo wasiliana nami kwa 0654726668.
Jacob Mushi
Mwandishi, Mjasiriamali na Mhamasishaji.
Simu: 0654726668
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com