Mtazamo wako juu ya Maisha ndio kila kitu. Yaani Maisha yako yako hivyo kwasababu ya mtazamo wako ulivyo.

Kuna msemo unasema maji ni uhai, Msemo huu ukiutazama katika yale matumizi na mahitaji yetu ya maji kila siku utaona ni kweli Maji ni Uhai. Ukitazama kwa ndani Zaidi utaona hata Maisha hayawezekani bila maji. Watu walioko jangwani ukiwaambia kwamba maji ni uhai watakuelewa vizuri sana kwasababu maji jangwani ni tatizo hayapatikani na wanayahitaji sana.
Hii ni kwasababu mtazamo wako umeuweka kwenye upande mzuri wa matumizi ya maji. Ukimleta mtu aliewahi kupata misukosuko ya maji. Mfano alienusurika kufa katikati ya ziwa au baharini ukamwambia bila maji hatuwezi kuishi anaweza asikuelewe. Kwasababu yay ale aliyopitia yeye ataona maji ni kifo sio uhai.
Kwa mitazamo hii miwili tunapata picha mbili tofauti kabisa juu ya maji. Hivyo basi katika Maisha yako usiishi kwa mtazamo mmoja tu. Usiyachukulie Maisha kwa mtazamo wako uliopo tu jua kabisa hata kama wewe unapitia shida kuna watu wengine wanafurahia Maisha. Kama wewe ndoa imekuwa chungu usitoe jibu la mwisho kwamba ndoa haifai bado kuna upande mwingine.
Maisha unayopitia usitumie kutoa majibu kwa wengine kwamba ndio Maisha yako hivyo. Kuna watu wanaumizwa kwenye mahusiano au ndoa, wanakuja huku nje na kutuaminisha wote kwamba ndoa ni mbaya sana, ndoa ni ngumu sana. Wengine watasema wanaume/wanawake hawaaminiki kabisa. Kumbe kile anachokisema ni sawa na mtu aliepitia dhoruba ya maji kwenye bahari akasahau kwamba huku nyumbani anahitaji maji kwa ajili ya kuoga.
Usiseme maji hayafai au ni mabaya sana kwasababu umepitia dhoruba baharini. Kuna watu wanahitaji japo hayo ya baharini wanayakosa. Usiseme Maisha ni magumu kwasababu ya hali unayopitia sasa hivi. Kuna mwingine hajui kama kuna hali hiyo unayopitia. Kuna mwingine pia anatamani japo angekuwa na Maisha kama yako.
Chochote unachopitia kisikufanye utoe jibu kwa watu wengine na kuwaaminisha kuwa ndio iko hivyo. Jaribu kufikiri kwa upande wa pili. Kama wewe umeona mahusiano yamekushinda usiupe ulimwengu jibu kwamba mahusiano hayafai. Kama ndoa imekushinda usjie huku nje kutuambia kwamba ndoa haifai bado wapo wengi sana wanafurahia ndoa zao.
#USIISHIE NJIANI.

Jipatie Nakala ya Kitabu cha Siri 7 za Kuwa Hai Leo, Wasiliana nami kwa 0654726668.

Jacob Mushi.
Mwandishi, Mjasirimali na Mhamaishaji
Simu: +255 654 726 668
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com  
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading