Vitu virahisi mara nyingi vinafanywa na wengi.  Kama jambo unalolifanya kila mtu anaweza kufanya jaribu kuangalia namna ya kujitofautisha au uachane nalo.

Kinachofanywa na wengi mara zote hakiwi na thamani kubwa. Kinachofanywa na wengi hakina matokeo makubwa.
Watu wenye mafanikio makubwa kuna vitu vya tofauti wanafanya ambavyo si kila mtu anaweza kufanya.
Kama unataka kuwa wa tofauti na kuleta tofauti kwenye jamii yako fanya vitu ambavyo sio kila mtu anaweza kufanya.
Fanya kitu ambacho wale watu wenye mawazo ya kawaida watakwambia huwezi,  kina fulani walishindwa.
Ukianzisha biashara yako halafu kila mtu akakuiga unatakiwa ujue kwamba hata watu wa kuwauzia watapungua.
Anza kufikiri tofauti na wengi wanavyofikiri. Kama wengi wanafikiri kwamba maisha ni kujenga,  kuoa/kuolewa na kusomesha watoto,  wewe fikiri mbali zaidi. Anza kufikiri juu ya kuacha alama,  kuliishi kusudi, kugusa maisha ya wengi. Usikubali kufikiri kama wengi wanavyofikiri.
#USIISHIE NJIANI
Usiache kusoma Kitabu cha Siri 7 za kuwa hai leo wasiliana nami kwa 0654726668.
Jacob Mushi
Mwandishi, Mjasiriamali na Mhamasishaji.
Simu: 0654726668
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading