HATUA YA 17: Tafuta mtu wa Kukukosoa.

Wanadamu kwa asili tunapenda kusifiwa. Pale inapotokea mtu amekukosoa wakati mwingine unaweza kufikiri anakuonea wivu au vingine. Lakini ukweli ni kwamba hatuwezi kukua au kuwa bora bila kupitia changamoto hii ya kukosolewa.

Mwandishi huyu anasema “Mjinga yeyote anaweza kukosoa, kulaani, na kulalamika lakini inahitajika tabia na kuweza kujidhibiti ili kuelewa na kusamehe. ~ Dale Carneige

Kwenye chochote unachokifanya kama hakuna wa kukukosoa inawezekana unakosea sana. Tunahitaji watu wa Kutukosoa ili tuweze kujifunza.

Ili ukosolewe lazima uende hatua ya ziada,  lazima ufanye jambo la tofauti kidogo na walilozoea watu.
Kama hukosolewi inawezekana Unafanya mambo yale yale kila siku. Yaani hakuna Ubunifu hadi watu wamekuzoea.
Jaribu kwenda hatua ya mbele zaidi kama hujaona watu wanakukosoa na wengine wakisema huwezi.
Unapokosolewa kubali na jifunze kwani hakuna mkamilifu duniani, hakuna aliezaliwa anajua kila kitu. Kila mwanadamu anakosea ndio maana wapo waliotuzidi kwa vitu mbalimbali ili kutuonyesha sehemu zile tunazokosea.
Bahati Nzuri sana ni kwamba watu wanaona Vizuri sana jambo unalolifanya kuliko wewe unavyoona. Watu wanatazama kwa sura nyingine tofauti na wewe unavyotazama.
Chukulia yale yote unayoambiwa katika mtazamo chanya. Tabasamu kabisa kwani ndio unakwenda kujengeka na kuwa mtu wa maana. Hata  kama anaekukosoa kafanya kwa makosa hakuna haja ya wewe kukasirika. Tambua tu ulilofanya limewagusa watu. Tambua pia kuna watu wanafuatilia unachokifanya kwa karibu.
Kumbuka: Kukosolewa ni lazima katika safari ya Mafanikio kama Unafanya jambo na wote wanakusifia kila siku unapotea. Kama Unachukia Kukosolewa utatumbukia shimoni. Wakati Mwingine wanaotukosoa wanaona sehemu zile tunazopita vyema.
Kubali Kukosolewa.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418

jacobmushi.com.
jacobmushi
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading