Kanuni ya kupata chochote kwenye maisha yako ni kuanza kukiona kwenye ufahamu wako. Hakuna chochote kinachotokea nje ya ufahamu wako. Watu wengi wamekuwa wanataka vitu ambavyo hawajaviona kwenye fahamu zao, wanatamani vitu walivyoviona kwa wengine.

Baada ya kutengeneza picha ndani yako lazima sasa uingie kwenye mchakato wa kufanya vitendo vya kuitengeneza picha yako kuwa halisi. Kuoana picha ndani yako ni kitendo cha Imani, Imani isiyo na matendo imekufa, kwa maana kwamba ukiwa na picha ndani yako na huna matendo ya kuifanya picha iwe halifi Imani yako imekufa. Usiishie kuwa na picha kubwa pekee yake ingia kwenye vitendo vya kuifanya picha iwe halisi.
Unaona picha ya kampuni kubwa unayoimiliki anza leo biashara ndogo kwa mtaji ule ulio nao. Haiwezekani kampuni ikatokea bila ya vitendo. Anza kujifunza na kusoma vitabu juu ya kile unachotaka kitokee.
Wakati unafanya vitendo kabla hujaanza kuona matokeo kuna changamoto nyingi sana. Ukubwa wa picha yako ndio unaongeza ukubwa wa changamoto utakazopitia. Usiogope changamoto kwasababu hakuna mtoto alieweza kusimama bila ya kuanguka hata mara moja. Hakuna alieweza kutembea bila ya kujikwaa.
Chochote unachokitaka kwenye Maisha yako anza kukiona ndani yako. Anza kutengeneza picha kubwa ndani yako. Ifanyie kazi picha hiyo kubwa bila ya kukata tamaa na mwisho wake itakuja katika uhalisia.
#USIISHIE NJIANI.
Jipatie Nakala ya Kitabu cha Siri 7 za Kuwa Hai Leo, Wasiliana nami kwa 0654726668.
Jacob Mushi.
Mwandishi, Mjasirimali na Mhamaishaji
Simu: +255 654 726 668
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com  

jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading